MICHEZO
Kocha wa AS Roma, Jose Mourinho amesema Josep Pep Guardiola amekuwa akitumia pesa nyingi kununua wachezaji huku akisikitishwa na klabu yake ya AS ROMA kushindwa kununua wachezaji kutokana na ukata.
Itakumbukwa siku za hivi karibuni Mkufunzi wa Manchester City, Pep Guardiola alipokiri waziwazi kwamba kiungo wake Kelvin Phillips anaweza kuondoka klabuni hapo mwezi ujao.
“Sio kwamba naona wivu ,lakini Manchester City walilipa euro milioni 80 kwaajili ya Kelvin Phillips na sasa Pep Guardiola amesema ni bora aondoke mwezi Januari. Kwahiyo ataondoka na watapata wachezaji mwingine .
Kwa upande wetu ni tofauti sana . Tungependa mchezaji mmoja , wawili ,watatu au wanne…. hata hivyo, sio rahisi kwetu kufanya hivyo. Tukileta beki mmoja ,Januari nitakuwa sasa na furaha.
Lakini ukiniuliza ikiwa ningependelea zaidi hayo ,bila shaka ningependa zaidi,lakini haiwezekani”.