HABARI KUU
Rais Yoweri Kaguta Museveni amezindua mfumo wa kielektroniki wa kulinda wawekezaji kwa jina la “EIPP” ambao utamwezesha Rais kufatilia Wawekezaji wa ndani na wa nje wakati wakifatilia mchakato wa kuwekeza kwenye nchi hiyo ya Mashariki mwa Afrika.
Jambo hili linajiri ikiwa ni baada ya kuwepo malalamiko ya wawekezaji kucheleweshwa katika michakato kwasababu ya kupitia Kwenye mikono ya watu. Mfumo huu wa “EIPP” unalenga kutatua changamoto hiyo huku ukimwezesha Rais kufatilia kila hatua ya mchakato.
Wawekezaji nchini Uganda wamekuwa wakilalamika kwasababu ya kucheleweshwa vibali na kukosa majibu kutoka kwenye mamlaka za serikali ambazo pia zimekuwa zikishindwa kutatua changamoto hizo na rushwa ikiwa inashamiri kwenye mchakato mzima.