HABARI KUU.
Kauli ya Papa Francis ya kuruhusu mapadri kuwabariki wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja imezua taharuki Duniani.
Kiongozi huyo wa Kanisa kubwa na lenye waumini wengi Duniani amesema sasa ni rasmi kwa Makasisi wa kanisa hilo kuruhusiwa kuwabariki wapenzi wa jinsia moja na wanandoa wasio wa asili.
Lakini msimamo wa Vatican unataja baraka hazipaswi kuwa sehemu za kawaida za taratibu za kanisa au zinazohusiana na miungano ya kiraia au harusi. Iliongeza kwa kutaja bado kanisa linazingatia ndoa kati ya mwanaume na Mwanamke ni halali.
Papa Francis ametangaza mabadiliko hayo siku ya jumatatu akiidhinisha mapendekezo ya Vatican 🇻🇦. Vatican inaweka uhalali wa jambo hili ikitaja kuwa Mungu ni wa wote,lakini Hati hiyo imewataka Makasisi kuzingatia kwanza mazingira ya walengwa .
Kwa mujibu wa Kanisa Katoliki, baraka ni maombi au ombi linalotolewa na mhudumu kama kasisi ,Askofu, Kadinali au Papa ambaye umuombea mhusika kwa Mungu na kuachilia maombi au ombi kwa mhusika huyo.
Mnamo mwaka 2021, Papa alitoa tamko kali akisema kuwa Makasisi hawawezi kubariki ndoa za jinsia moja kwasababu ni dhambi mbele za Mungu.
Sehemu mbalimbali Duniani baadhi ya Maaskofu walikuwa tayari wamewaruhusu Makasisi kuwabariki wapenzi wa jinsia moja ingawa haukuwa msimamo wa kanisa kwa ujumla.
Mwezi wa Oktoba, Papa alikuwa tayari kutoa msimamo wa kanisa katoliki kuhusu watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja na waliobadili jinsia zao kutokana na shinikizo kutoka kwa baadhi ya Makadinali wa kanisa hilo.