0:00
MICHEZO
Klabu ya West Armenia inayoshiriki ligi kuu ya Armenia 🇦🇲 imevunja mikataba ya wachezaji wawili raia wa Tanzania, Yusuf Athuman na Erick Mwijage kwa makubaliano ya pande zote mbili.
Yusuf alijiunga na klabu hiyo akitokea Young Africans SC ya jiji Dar es salaam huku Mwijage akitokea klabu ya Kagera Sugar ya Mkoani Kagera.
Nyota hao wamepewa mkono wa kwaheri baada ya Ligi kuu ya Armenia kumalizika huku timu hiyo ikimaliza nafasi ya 8 kati ya timu 10 ,alama 17 katika mechi 20 ,ikishinda 5, sare 2 na kupoteza mechi 13.
Related Posts 📫
CELEBRITIES
Music producer Young John posted a video on social...
The 26-year-old Belgium international only joined the French side in...
CHICAGO — Jordan Love and the Green Bay Packers made...