HABARI KUU.
Wagombea 16 wamejitokeza kuchuana na Rais Vladimir Putin kwenye uchaguzi utakaofanyika mwezi Machi 2024.
Hayo yamesemwa na maafisa wa uchaguzi leo Desemba 20,2023.
Kwa siku za hivi karibuni imezoeleka Urusi kutohusisha wapinzani kwenye chaguzi hali ambayo imekuwa ikifanya hali ya kisiasa kuwa mbaya na hali iliyochangia Kremlin kuivamia Ukraine kijeshi mnamo mwaka 2022.
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi (CEC) amenukuliwa akisema:-
“Kufikia sasa,tumepokea maombi kutoka kwa wagombea 16 katika uchaguzi wa urais “
Amesema Ella Pamfilova akinukuriwa na chombo cha serikali cha RIA Novosti.
Ikitokea Vladimir Putin akashinda uchaguzi mkuu huu,atakuwa anaiongoza Urusi kwa muhula wa tano .
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.