MICHEZO
Mahakama kuu ya umoja wa Ulaya imetoa uamuzi kuhusu sakata la mashirikisho ya UEFA na FIFA kupinga kuanzishwa kwa michuano ya “European Super League “ikidai kuwa UEFA na FIFA zilikiuka sheria ya mashindano.
Kwa muktadha huo sasa ni rasmi European Super League imeshinda kesi dhidi ya UEFA ambaye ameelezwa kwamba hana udhibiti wa moja kwa moja kwenye kila maamuzi wa mpira wa miguu . Sasa ni rasmi Super League inaweza kupanga mashindano yake bila kuingiliwa na yeyote.
Mkurugenzi Mtendaji wa A22 Sports amesema :-
“Tumeshinda haki ya kushindana . Ukiritimba wa UEFA umekwisha. Kandanda ni bure. Vilabu sasa viko huru dhidi ya vitisho na vikwazo na viko huru kuamua mustakabali wao wenyewe”.
Amesema Bernd Reichart.
Aidha Bwana Reichart amewaomba na kuwahak8kishia mashabiki kwamba wataangalia michezo bure na pia akitoa hakikisho kwa vilabu kupata mapato .