HABARI KUU
Wanafunzi wa Korea Kusini wamefungua kesi dhidi ya serikali baada ya mtihani wao wa kujiunga na chuo wa masaa nane kumalizika ndani ya sekunde 90 (dk 1:30) mapema zaidi ilivyotarajiwa.
Wanafunzi hao wanadai fidia ya won 20 million sawa na Tsh milioni 38.1 kila mmoja. Sawa na gharama ya mwaka mmoja wa masomo ,kwaajili ya kufanya mtihani tena, baada ya msimamizi kugonga kengele kimakosa.
Kim Woo-Suk ,wakili anayehusika na utetezi wa wanafunzi, aliviambia vyombo vya habari kuwa maafisa wa mtihani hawakuomba radhi kwa hilo. Huku taarifa za ndani zikieleza kuwa kosa hilo lilifanyiwa na msimamizi ambaye alikosea kusoma muda.
Suneung ni miongoni mwa mtihani mgumu sana ambayo huamua hatma ya nafasi za chuo kikuu,kazi,na hata uhusiano wa siku zijazo . Ambao hufanyika kwa masaa matano mpaka nane .
Wanafunzi hao wanasisitiza haki yao,kufuatia kosa hilo linaloweza kuathiri maisha yao ya baada.