HABARI KUU
Kulala kwa muda mrefu zaidi wikiendi kunaweza kusaidia kuboresha afya yako ya moyo,mishipa na kupunguza hatari ya mshtuko wa moyo ,kwa mujibu wa tafiti.
Utafiti,uliofanywa na Watafiti wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Nanjing nchini China, ulichambua muda ambao washiriki walilala wakati wa wiki na wikiendi, huku wakikusanya taarifa kuhusu ikiwa walikuwa na ugonjwa wa moyo,shinikizo la damu au kisukari.
Ambao waliolala kwa walau saa moja zaidi ya mwishoni zaidi mwa wiki kuliko siku za wiki walikuwa na viwango vya chini vya magonjwa ya moyo ikilinganishwa na wale ambao hawakufidia usingizi wao.