MAMBO 10 YA MSICHANA ANAYEKUPENDA

0:00

MASTORI

Duniani kila mmoja wetu angetamani kuwa na mtu anayeendana nae na kupenda na hata ikiwezekana kuwa nae kwenye maisha ya ndoa.

MSICHANA

Pamoja na mambo mengine mengi ,wengi tumejikuta hatufahamu kwa usahihi ni wapi watu wetu? Sasa leo ebu tuone ,

ISHARA 10 ZA MSICHANA ANAYEKUPENDA KWA DHATI

1. WIVU. Msichana mwenye mapenzi na wewe atakuwa na wivu. Jihadhari sana kuwa na mahusiano mengine utamuumiza.

2. SIKU YA KWANZA ANAPENDA KUKUONYESHA UZURI WAKE. Hapa kuna mambo mengi,siku hii hata kama ni mdogo wa umri atahitaji kuonyesha ukubwa au ujuzi wake wa mahaba. Hapa kama kijana, unatakiwa kumpa uhuru akufanyie anavyoweza.

3. AOMBI HELA YAKO. Msichana anayekupenda anafahamu fika, kuomba hela ni kama atakupoteza sana sana atapenda kukushirikisha kwenye mahitaji yake badala ya kuomba hela moja kwa moja.

4. ANAKUNUNIA . Hapa sio chuki za jumla au kuwa na kinyongo isipokuwa hapa anataka kusikia unamuomba tu msamaha . Mara nyingi, hapa mtoto wa Mama mkwe utamuona kama ana hasira au kachukia lakini hayo ndiyo “mapozi”.

5. ANAPENDA KWELI. Upendo huu ni wa hatari mno kwani siku ukimkosea anaweza kukuchukia maisha yako yote. Angalizo,fahamu aina ya Upendo huu.

6. HANA MAHUSIANO ZAIDI. Hii ni ishara ya Mwanamke wa ndoa,ukiona ishara hii ya msichana ,fahamu ya kwamba yuko na wewe pekee.

7. ANA MOYO WA YAI . Moyo huu ,amekukabidhi wewe na anaamini wewe unatembea nao kwa usalama.

8. ANAPENDA KUKUSHIRIKISHA MIPANGO YA MAISHA YAKE. Huyu mara nyingi atakupa hata siri za familia yao au atakwambia anahitaji uwe kama baba yake anavyompenda mama yake. Binti wa aina hii mshikilie sana.

9. MWENYE HISIA KALI ZA MAHABA. Kwa msichana ambaye hajawazoea wanaume, ukimkumbatia na hata kumpiga busu anahisi kuchanganyikiwa tofauti na ambaye amezoea hayo mambo.

10. HANA MAMBO MENGI. Kuna wasichana wanavuta sigara ,kunywa Pombe na wanavaa nusu uchi. Msichana ambaye hana mambo huenda ukiwa nae anamaanisha mapenzi ya kweli.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

See also  DUNIA INGEKUWA NZURI KAMA TUNGEKUWA NA WANAWAKE HAWA

Related Posts 📫

Dodgers and fans relish festive World Series...
LOS ANGELES, - The Los Angeles Dodgers celebrated their World...
Read more
SERIKALI YAAGIZA MAMLAKA ZOTE KUHUSU UVUNAJI MAJI
HABARI KUU Serikali imeziagiza Mamlaka za Maji kushirikiana na Halmashauri...
Read more
Russia's Valieva plans to resume career after...
Russian figure skater Kamila Valieva plans to resume her competitive...
Read more
URUSI YAFANYA MAJARIBIO YA NYUKLIA ...
HABARI KUU. Urusi imefanya "Jaribio la mwisho lililofanikiwa" la kombora...
Read more
Super Salah sends Liverpool top with victory...
LIVERPOOL, England, 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 - A sensational trademark strike from Mohamed...
Read more

This Post Has One Comment

Leave a Reply