NAPE KUSHUGHULIKA NA WALIOZUSHA KIFO CHA MPANGO

0:00

HABARI KUU.

Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ,Nape Moses Nauye amesema hatua zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria kwa wale waliohusika na kutangaza uvumi wa kifo cha Makamu wa Rais, Dkt. Philip Isdor Mpango kwenye mitandao ya kijamii.

Waziri Nape ameyasema leo Desemba 10,2023 katika ukurasa wake wa X muda mchache baada ya Makamu wa Rais kutoa kauli ya kuwasihi Watanzania kutumia vizuri mitandao ya kijamii na kuachana na habari za uzushi.

Dkt. Mpango hakuwa ameonekana hadharani kwa takribani mwezi mmoja jambo ambalo sio kawaida kwa kiongozi mkuu nchini huku tetesi zikidai anaumwa na nyingine zikisema amefariki Dunia.

Nape amesema ameelekeza vyombo vyote vinavyohusika kuchukua hatua ili iwe mfano na kujenga jamii inayoheshimu uhuru wa kila mtu.

“Pole Mhe. Makamu wa Rais, tumekusikia. Kwakuwa tuna sheria zinazoelekeza mitandao itumike vizuri na kwakuwa tuna taasisi na watu wa kusimamia sheria hizi,bila kuathiri uhuru wa watu ,tutachukuwa hatua kutokomeza matumizi haya mabaya ya mitandao! Naamini wote watatuelewa!

Uhuru wowote unaoingilia uhuru wa mwingine ni uvunjifu wa sheria ,hatuwezi kujenga jamii inayoona jambo hilo ni la kawaida”.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

TOP FIVE RICHEST COUNTRIES IN THE WORLD
The top 5 richest countries in the world based on...
Read more
AINA ZA UTE UKENI NA MAANA YAKE
Ute ukeni hutofautiana kwa rangi, muonekano, na harufu kulingana na...
Read more
Sababu za Kujifungua Mtoto Mwenye Uzito Pungufu
USIVUTE SIGARA WAKATI WA UJAUZITO SABABU ZA KUZAA MTOTO MWENYE UZITO...
Read more
FAMILIA YAKAA PORINI MIEZI 2 IKISUBURI NDUGU...
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
Conor Gallagher is expected to return to...
The England international, 24, was pictured in the La Liga...
Read more
See also  CCM YAMPIGA CHINI DANIEL CHONGOLO

Leave a Reply