HABARI KUU
Kwa mara ya kwanza baada ya karne moja Nchi ya Ukraine itasheherekea Sikukuu ya Christmas tarehe 25 Desemba mwaka huu tofauti na utaratibu uliozoeleka wa sherehe za Kirusi wa Januari 7 ya kila mwaka.
Ukraine itasheherekea Sikukuu za Christmas kwa mwaka huu kwa kufuata kalenda ya Gregorian ,pamoja na Wakristo wengi Duniani na kuachana na utaratibu wa Urusi ambao huwa wanasheherekea kila ifikapo Januari 7 .
Mnamo Julai mwaka huu Serikali ya Ukraine ilipitisha sheria iliyosainiwa na Rais Volodymyr Zelenskyy ya Mabadiliko ya tarehe hiyo ikilenga kupuuzia utaratibu wa kanisa la Othodoski la Urusi ,ambalo linafuata kalenda ya Julian.
Nchini Ukraine, Wakiristo ni wengi pamoja na kuwa made madhehebu ya Othodoski yamekuwa ni ya muda mrefu nchini humo.
Related Content
yandanxvurulmus.M1GDXAJBJKsa