HABARI KUU.
Askofu wa jimbo kuu la Geita, Flavian Kassala amesema hayuko tayari kubariki ndoa zilizo kinyume na maadili kwani ni kinyume na maagano ya Mwenyezi MUNGU ya kutaka binadamu wazaliane na kuendeleza vizazi Ulimwenguni.
Askofu Kassala amesema bora abariki jiwe ukajengee nyumba na sio kubariki mambo yaliyo kinyume na maadili.
Akihubiri katika Misa ya kitaifa ya Krismasi ,amesema ndoa zisizo na maadili ni kwenda kinyume na maandiko ya Mungu yanayotaka binadamu kuzaliana.
Amesema binadamu anakataa uumbaji wa Mungu na kufanya mambo yaliyokatazwa huku wakitaka kanisa libariki jambo ambalo amelipinga vikali.
“Binadamu amemuacha Mungu na kufanya mambo yaliyochukizo.Binadamu amekataa uumbaji na kuendeleza uumbaji na sasa wanafanya mambo machafu yasiyompendeza Mungu ,wamekuwa wakiharibu kizazi kwa kutoa mimba sana na sasa wanataka tubariki ndoa zisizo na maadili. Kwangu bora nibariki jiwe lakini sio uchafu huo”.
yandanxvurulmus.jUFalQuWk8K7
synthroid 100 pill
daily prednisone