NYOTA WETU.
Mwanamziki na mfanyabiashara wa Marekani, Kanye West ametoka hadharani na kuiangukia jamii ya Wayahudi ambayo awali alikuwa ameitolea maneno makali hasa akihishtumu kwa maneno yake makali ambayo yaliibua hasira kwa jamii hiyo.
Kanye West anakiri wazi hakuwa na lengo baya na anaonekana kusononeshwa na kauli zake na anakiri wazi kwa jamii hiyo ya Wayahudi kwamba amekosea.
Msanii huyo ambaye kwasasa anajiita Ye aliandika kwenye mtandao wake:-
“Naomba radhi kwa jamii ya Wayahudi kwa yaliyotokea ,maneno au matendo yangu. Haikuwa nia yangu kuumiza au kudhalilisha ,na ninajutia sana maumivu yoyote ambayo huenda niliyasababisha”.
Kanye West hajaishia hapo ,ameendelea na kusema:-
“Msamaha wako ni wa muhimu kwangu, na nimejitolea kufanya marekebisho na kukuza umoja”.
Chapisho la Bwana Ye lilizua sintofahamu na kumsababishia hasara kubwa hasa pale alipopoteza udhamini mkubwa wa kampuni ya Adidas.