MICHEZO.
Ligi kuu ya England haijawahi kuwa na mwamuzi mweusi tangu ,Uriah Rennie aliyekuwa mwamuzi pekee mweusi katika historia ya mashindano hayo hadi kufikia jana,Desemba 26,2023 ambako mtu mweusi mwingine ameonekana.
Sam Allison
Sam Allison, ambaye alikuwa mwamuzi wa mechi kati ya Sheffield United na Luton Town ,amekuwa mwamuzi pekee mweusi kuchezesha ligi ya England baada ya kupita miaka 15 tangu mwaka 2008,Uriah Rennie alipostaafu .
Bwana Rennie alichezesha michezo mingi kwenye ligi hiyo pendwa kwa takribani misimu 11 na sasa hatua nyingine imepigwa kwa uwepo sasa wa mtu mweusi mwingine Bwana, Sam Allison.
Uriah Rennie