NYOTA WETU.
Licha ya Cardi B kuthibitisha kutengana kwao mapema mwezi huu ,imeonekana wawili hao waliungana kusheherekea sikukuu za kuzaliwa kwa Masiha na watoto wao wawili Kulture na Wave.
Kuachana kwao kulifahamika ni baada ya Cardi B kuweka maudhui kwenye mtandao wake wa Instagram, huku ikitajwa kwamba Offset ndiye chanzo cha kuachana baada ya kutoka na Mwanamke mwingine.
Mashabiki walilipuka baada ya kuona video iliochapishwa na Cardi B akiwa yeye na Offset na watoto wao. Mashabiki walifurahi,kwani walidhani wawili hao wameweka tofauti zao pembeni na kuamua kurudiana.
Cardi B, amenukuliwa akisema :-
“Najua leo imekuwa siku ya matukio sana, sifikirii kuhusu hivyo. Sijali kuhusu hata mojawapo linapokuja tukio la siku ya leo,sifikirii kama ni kweli, nimekuwa pekee yangu kwa muda sasa. Nimeogopa kuwa muoga,sijui niiambieje Dunia, lakini nahisi leo imekuwa ishara”.