MAPENZI
Kila kitu kikifanyika kwa kiasi huwa akihumizi au kuwa na madhara. Sasa leo tuangalie mambo matano pekee ambayo ni hatari kwa mwanaume kumfanyia Mwanamke:-
1. KUMSOMESHA MWANAMKE.
Labda tu awe ni mkeo ,kusomesha ni jukumu la wazazi au walezi. Sio vibaya kumsaidia kwa mahitaji ya hapa na pale lakini kubeba jukumu Zima la kusomesha,hiyo haiko sawa. Ukiamua kusomesha, ni juu yako lakini usiwe na matumaini kwamba kusomesha ndio umejiwekezea. Watu tunabadilika na hata yeye anaweza kubadilika akaolewa na mtu mwingine.
2. KUTENDA UHALIFU KWASABABU YAKE.
Ukigundua maisha yake ni ya gharama ambayo wewe huwezi kuyamudu,usiende kuiba au kufanya tukio ilimradi uwe nae. Kama ana mapenzi ya kweli kwako hataweza kukupunguzia presha hiyo au matumizi yake ya gharama.
3. KUJIWEKA KWENYE WAKATI MGUMU KISA YEYE.
Kama kuna jambo la lazima unaweza kufanya hivyo lakini kama sio hivyo ebu kuwa mbinafsi kwaajili ya maslahi yako. Utakuwa mtu wa ajabu,umtumie yeye hela ya kula wakati wewe hujala au umpe hela ya kusuka na wewe unadaiwa hela ya pango.
4. KUSAHAU NDOTO ZAKO.
Kabla ya kumuona ,kumbuka ulikuwa na ndoto zako pale unapogundua yeye ni kikwazo cha kufikia ndoto unaweza kuachana nae. Uliweka mipango na malengo ya kwenda kusoma nje ya nchi lakini yeye anakwambia utamwachaje? Endelea na malengo yako na kama atakuwa wako atakusubiri.
5. KUIKOSEA FAMILIA YAKO ADABU KISA YEYE.
Wanawake wana tabia fulani ya kutaka kukuweka kwapani hasa anapogundua unampenda kupitiliza. Hata,anaweza kuthubutu kuamrisha ndugu na hata wazazi wako wasije kwako. Usiruhusu jambo hili,familia yako ni kila kitu.