TABIA ZA MWANAUME AMBAYE HAJAKOMAA KIAKILI KWENYE NDOA

0:00

MAPENZI

1. ANAYEZILA CHAKULA.

Bwana Mkubwa, unampa mkeo hela ya kununua chakula na chakula kikipikwa na kuletwa unakataa kula! Hii ni tabia ya utoto,ni muda wa kukuwa sasa hakuna sababu yoyote ya kukufanya uwe hivyo. Unaweza kuwa na hasira lakini hazitakiwi kuwa za kuvuka mipaka,kuzila chakula ni ishara mbaya.

2. KUMWAMBIA MKEO KILA MARA KUWA WEWE NI KICHWA.

Nikwambie tu siri,hata ikitokea mkeo akakukosea adabu anajua fika wewe ni kichwa. Kwahiyo suala la kusema wewe ni kichwa sio la kutamba nalo. Usitumie nguvu kubwa ujulikane kuwa wewe ndiyo mwamba. Wanaume wakomavu hawana hii hulka.

3. VITISHO.

Kumpiga Mwanamke au kumtisha mkeo kwamba unaweza kuoa Mwanamke mwingine ni ishara ya utoto . Mwanaume mkomavu ni mwepesi muno wa kuzuia mkono wa ngumi na ni mwepesi mno kuzuia ulimi wake. Ni kweli Mwanamke anaweza kufanya jambo la kitoto lakini wewe kama mwanaume, simama kama mzazi mwenye hekima na busara.

4.KUMSHITAKIA MKEO KWA MARAFIKI NA NDUGU.

Mkeo akikosea ,msahihishe lakini sio vizuri akikosea unapeleka habari kwa ndugu, jamaa na marafiki. Kumtangaza mkeo ni kumshusha hadhi ambayo itamfanya kupoteza thamani yake kwenye jamii na thamani ikishuka ni ngumu kuirudisha.

5. ANAYEENDEKEZA UHUNI.

Ameoa kweli lakini bado anaweza kumtusi mke wake mbele za watu au hata kutisha kumpiga mke wake. Kufanya hivi hata kama umeoa ,wewe utakuwa ni “mvulana” na sio mwanaume. Nyumba ya mtu wa aina hii ni matusi mwanzo mwisho.

6. SIO MSAIDIZI.

Ni aibu Mwanamke kuwa na kazi nyingi ndani na wewe kama mwanaume upo unaangalia zako TV na huna habari nae. Mwanaume ni vizuri afahamu wapi amsaidie mke wake kwa kuwa ,ndoa ni yenu na familia ni yenu lazima mshirikiane kuijenga. Mwanaume ambaye sio msaada kwa mke wake hata akiwa ana shida,huyu bado ana utoto mwingi.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

See also  MAMBO 7 AMBAYO MWANAUME HUVUTIWA NAYO KUTOKA KWA MWANAMKE

Related Posts 📫

MUDA SAHIHI WA KUSHIRIKI TENDO LA...
MAPENZI Hii ni kwa walioko kwenye ndoa pekee . Wakati sahihi...
Read more
MBINU 10 ZA KUONGEZA WINGI WA MBEGU...
Mwanaume mwenye uwezo wa kuzalisha anahitaji kuwa na mbegu zisizopungua...
Read more
Men’s doubles shuttlers Aaron Chia-Soh Wooi Yik...
Aaron-Wooi Yik have made the cut for the prestigious season-ending...
Read more
ANGELINA JOLIE AISHUTUMU ISRAEL ...
NYOTA WETU Muigizaji mkongwe na mshindi wa tuzo za Oscar...
Read more
Maresca will bring half of Leicester to...
According to The Telegraph, Chelsea intend to treat Leicester City...
Read more

Leave a Reply