DiscoverCars.com                                                                       

AINA 12 ZA WANAUME NA TABIA ZAO.

0:00

MAPENZI.

Wanaume wamegawanyika katika matabaka kadhaa,sasa unaweza kumtambua mumeo ni yupi ? Au wewe kama mwanaume huko kwenye kundi lipi?

1. MWANAMUME MGUMU.

Huyu ni mwanaume mwenye majivuno,mkaidi na asiyetikiswa. Ni mwanaume asiye shaurika au kusahihishwa . Hana woga kwa yeyote na hana heshima hata kwa ndugu wa mke wake na mtu ambaye kuishi nae ni vigumu.

2. MWANAUME BANDIA.

Ni mzuri kitandani na mzuri wa kupenda kula vizuri ni mvivu asiyejishughulisha . Ni mvivu ambaye hata familia haijali.

3. MWANAUME KAPERA.

Ni mwanaume anayemuacha mke wake kwenye chumba. Anayeishi kama yuko pekee yake . Ni mwanaume mbinafsi.

4. MWANAUME ASIDI.

Huyu ni mtu wa hasira ,mtu wa ngumi mfukoni. Hana utani,hacheki,hana masihala . Nyumba yake ni kama “KAMBI YA JESHI” yeye ni kama Simba ndani ya nyumba.

5. MSIMAMIZI WA MTUMWA.

Ni mwanaume anayeamini kuwa mwanamke ni mtu wa kuchungwa . Pia anajua Mwanamke ni mtu wa kupika,kufua, mashine ya kufanyiwa ngono,Kiwanda cha kufyatua watoto na mfanyakazi wa ndani. Anayeipenda familia yake kuzidi mke wake na mke wake atakiona cha moto akiwa ni Mwanamke wa kuzaa wasichana pekee.

6. MWANAUME JUMLA.

Huyu ana mnyororo wa marafiki wa kike,malaya, na wanawake wapya wapya. Anatembea na kila mtu ,wakiwemo hata ndugu wa mke wake na hata wafanyakazi wa ndani.

7. MWANAMUME MKAVU.

Hana ukaribu na mke wake “Hakuna upendo,Hakuna mahaba wala hana kubusu” . Mwanamke wake lazima abishe hodi ndio aingie chumbani mwake. Ni mgumu kuongea na mke wake na hana heshima kwa mke wake hata mbele ya wageni.

8. MWANAUME PANADO.

Huyu ni aina ya mume ambaye huwa anachukua alichonacho mke wake na kukitumia kwa maslahi yake.Huyu anamtumia tu mke wake kwa faida zake na huwa hana upendo kabisa.

9. MUME KIMELEA.

Huyu hafanyi kazi,mvivu na asiyewajibika . Hawezi kumsaidia mke wake ili nae mke aone unafuu. Ni mwanaume anayemfanya mke wake aumize kichwa. Kiufupi ni wa kumpa mke wake msongo na kufanya mke wake aishi kwa msongo.

10. MUME MTOTO.

Huyu ni mwanaume ambaye anaweza hata kususa kula kwasababu ana hasira. Ana hulka za kutaka kumfukuza mke wake na wakati mwingine huwa anamlinganisha mke wake na wapenzi wake wa zamani. Ni mwanaume, ambaye anampenda mama yake mzazi kuliko mke wake na ni mwanaume ambaye huwa anatoa siri za ndani ya nyumba yake na kuwaeleza jamaa na marafiki zake.

11. MWANAUME MTEMBEZI.

Huyu ni mwanaume anayehudumia vizuri tu lakini hana muda na familia yake . Yeye uja nyumbani kama mgeni.

12. MWANAUME MCHA MUNGU .

Ni mwanaume anayewajibika . Ni mwanaume mwenye hofu ya MUNGU. Ni baba, Kiongozi na rafiki wa mke wake na watoto wake. Ni mume mwenye upendo.

See also  MAMBO 11 AMBAYO MABINTI WENGI UDANGANYWA NAYO ILI WATOE MZIGO <!--INDOLEADS - END-- >

By juniitv

JUNIITV

Leave a comment