HABARI KUU.
Mkosoaji wa Serikali ya Kigali wa muda mrefu, Anne Rwigara amefariki Dunia kwa kinachotajwa na mama yake mzazi kuwa ni kifo chenye utata.
Anne ambaye ni dada wa Diana Rwigara, mwanasiasa aliyetaka kuwania urais wa Rwanda mnamo mwaka 2017 kabla ya kuzuiliwa na tume ya uchaguzi ya nchi hiyo, ameaga Dunia akiwa nyumbani kwake, California nchini Marekani ambako inatajwa kabla ya umauti wake alikuwa akilalamika maumivu ya tumbo.
Mwanamke huyo aliyefariki Alhamisi ya Desemba 28,2023 akiwa na umri wa miaka 41 ,alikuwa ni binti wa mfanyabiashara wa nchini Rwanda, Assinapol Rwigara.
Mfanyabiashara huyo,alifariki kwenye ajali yenye utata mnamo mwaka 2015 na miaka miwili baadae ,familia yake yote,akiwemo mjane na wanae ,Anne na Diana, walikamatwa na kufunguliwa mashtaka ya ukwepaji kodi na hatimaye walifungwa.
Bi .Adeline Rwigara amenukuliwa akiseama kifo cha binti yake kina utata kwani hakuwa anaumwa.
Kufuatia habari ya kifo cha mwanadada huyo mrembo,mitandao ya kijamii ilijawa na hisia za watu ambao waliishtumu serikali ya Kigali kuhusika na kifo hicho.