HABARI KUU
Akizungumza kwenye mkutano mkuu wa mwisho wa mwaka wa wana Dayosisi ya Kaskazini, waishio nje, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa ,Aggrey Mwanri amesema zinahitajika jitihada za makusudi za serikali, jamii na hata kanisa kumaliza tatizo la ulevi mkoani humo, kwani nguvu kazi ambao ni vijana wanapotea.
Naye,Askofu wa kanisa hilo la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Mstaafu, Dkt. Fredrick Shoo ,ambaye pia ni mkuu wa Dayosisi hiyo amesema chanzo kikuu cha ulevi Mkoani humo ni ukosefu wa ajira kwa vijana na akaenda mbali kwamba hata matumizi ya bangi na dawa za kulevya yanachangiwa na vijana wengi kukaa vijiweni.
“Tusipojitahidi kuondoa tatizo hili ,hata sisi tulio watu wazima tutahathirika kwa namna mbalimbali ikiwemo usalama wa familia zetu na mali tulizo nazo huku nyumbani “.