MAPENZI
Kuwepo kwa mitandao ya kijamii kumesaidia na pia kuharibu baadhi ya mambo hasa kwenye suala la mahusiano.
Siku hizi mambo ni rahisi muno,kipindi cha nyuma kabla ya mitandao ya kijamii, hisia zilielezwa waziwazi kama vile: Kulia,kucheka au hata hasira.
Siku hizi za Facebook, TikTok, Instagram na WhatsApp mapenzi ni rahisi kwani mtu anaweza kutuma meseji akiwa na hasira lakini anayeipokea akaipokea kwa furaha au kuna mazingira mengine ambapo mtu anaweza kuwa na hisia za kweli lakini anayetumiwa ujumbe asielewe hisia hizo. Sasa tuone SENTENSI 5 ambazo Wanawake wengi huvutiwa nazo.
1. WEWE NI MREMBO.
Kila Mwanamke anapenda kusikia akiambiwa alivyo Mrembo au alivyo na sura nzuri. Kumvuta ,Mwanamke akupende, weka kwenye akili kwamba kusema hivi ni kushawishi tosha.
2. UNA TABASAMU NYORORO au MURUA.
Kweli ukiwa na nia ya kumpata Mwanamke basi usisite kumsifia kwa jinsi anavyotabasamu kwa ulaini wake. Kila Mwanamke anapenda kusikia,yeye ni mlaini fulani. Hii inatokana na kwamba wanawake wanapenda kulindwa.
3. UNAJISIKIAJE
Hii sentensi lazima iendane na kwanza,uwe umefahamu hali yake labda kwa siku hiyo yuko tofauti. Usisite kumjulia hali na ikiwezekana kumsaidia anapokuwa ana kitu kinamtatiza. Kufanya hivi ,humfanya Mwanamke kujiona ana thamani mno .
4. NILIKUWA NAKUWAZA.
Hakuna shaka,maneno haya huwa yanaleta faraja kwa Mwanamke na huwa yanampa shauku ya kutaka kujua ulikuwa unamuwaza kwasababu gani? Kwa hili basi litafanya ukaribu wake na wako uwe mkubwa.
5. NAKUTAMANI.
Kusema ukweli, hakuna kificho bila kutamani huwezi kumpenda Mwanamke. Unaweza kutamani miguu,makalio,sura,macho,rangi ya ngozi,sauti na hata tabia zake yote haya ni tamaa. Tamaa ndio msingi wa upendo kutoka kwa mwanaume kwenda kwa Mwanamke.