HIZI NDIO SIFA ZA MWANAMKE WA KUOA.DiscoverCars.com

0:00

MAPENZI.

Kuna tofauti kati ya “Mwanamke ” na “Mke”. Mke , ni yule mwenye jinsia ya kike kwa asili ya kuzaliwa.

Mwanamke ni mwenye maumbile ya kike na mwenye haiba ya kuolewa au kuishi na mwanamume katika ndoa.

Utofauti kati ya Mwanamke na Mke ndio huleta tofauti hata kwenye mahusiano kwani kuna mwenye sifa za kuolewa na mwingine hana.

HIZI NI SIFA ZA WANAWAKE

1. Mwanamke ni mtu wa kumpa matumaini mume wako na kamwe sio mkatisha tamaa.

2. Mwanamke sio mtu wa kumshurutisha mume wake kutumia pesa zote bali ni mtu wa kumsihi mume wake kuweka akiba.

3. Mwanamke sio mtu wa kumkashfu au kumtusi mume wake bali maneno yake humponya mume wake.

4. Mwanamke anajua ni muda upi wa kuongea na ni muda upi wa kunyamaza.

5. Mwanamke ni mwenye kuweka akiba au siri ya maneno. Anajua kuna leo na kesho.

6. Mwanamke hawezi kuuza utu wake ili apate hela ya kusuka au kununulia vitu vya thamani, kwasababu anajua yeye ni wa thamani.

7. Mwanamke ni mwangalizi na mtuzaji wa tumbo lake maana, tumbo limebeba kizazi

8. Mwanamke ni kama Malkia,hana haraka ya mambo.

9. Mwanamke ni ambaye hata akiwa kwenye mahusiano na mtu sio wa kufuja hela bali anampa busara tu mwanaume

10. Mwanamke ni yule anaefahamu upekee aliokuwa nao ambao unamtofautisha na mwanamume

11. Mwanamke ni yule ambaye hata mume wake akilia ,sio mwepesi wa kumshusha thamani bali atamzingatia.

12. Mwanamke sio wa kula hela za mwanaume kwa kisingizio cha kuwa kwenye mahusiano.

13. Mwanamke ni mtu anayefahamu kilichomfanya mume wake ampende,na hicho ndicho ataendelea kukiboresha zaidi

14. Mwanamke sio Jehanum bali yeye ni sehemu ya faraja kwa mume wake

15. Mwanamke anatambua kuwa uwepo wa mume wake ndio heshima na nguvu kwake.

16. Mwanamke ana akili,hufanya maamuzi sahihi kwaajili yake na kwa jamii yake. Mwanamke ndio taifa na Dunia.

Mwanamke sio Mke,yeye ndio huitwa Mrembo haijalishi kwa muonekano wa sura au ukubwa wa makalio.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Late Bowen penalty gives West Ham dramatic...
LONDON, - Jarrod Bowen converted a controversial last-gasp penalty to...
Read more
HIKI NDICHO KIMEMKWAZA MWAKINYO ...
Michezo Hassan Mwakinyo ameingia kwenye mzozo na promota wa pambano ...
Read more
National grid experiences another significant failure in...
In a troubling development for Nigeria, the national power grid...
Read more
UTI KWA WANAUME
Uti kwa wanaume maambukizi ya mfumo wa mkojo kwa wanaume...
Read more
8 REASONS WHY MEN BREAK UP WITH...
The end of a relationship can feel like the end...
Read more

Leave a Reply