MAMBO 5 AMBAYO HUTAKIWI KUMUOMBA MWANAMKE ANAYEKUPENDA

0:00

MAPENZI

Mahusiano mazuri yana mambo mengi mazuri kati ya wawili wapendanao na huwa yanaenda tu yenyewe bila kutumia nguvu.

Pale mwanaume au kijana unapokuwa sehemu sahihi ya mapenzi basi haya mambo huwa hayahitaji nguvu au ushawishi wako.

1. KUTUMIWA PICHA.

Unapokuwa na mpenzi wako,suala kutumiwa picha sio la kuomba bali linakuja lenyewe kwasababu kutumiana picha ni sehemu ya mawasiliano na kuweka ukaribu wa mawasiliano yenu. Kwa unyeti wa mawasiliano, kila mara picha za matukio ya mpenzi wako zitatumwa hata bila ya kuuliza au kuomba.

2. KUWA NA MUDA WA PAMOJA.

Suala la muda wa kukaa na kuongea au kutoka wote pamoja huwa alihitaji kuombwa kwani ,Mpenzi wako atakupa muda huo . Matendo yenyewe yanaongea zaidi kuliko maneno.

3. KUJIBIWA JUMBE.

Meseji zako zitajibiwa kwa wakati kwasababu hata mpenzi wako anatambua thamani ya mawasiliano. Wengi wa wanaume huwa wanapata wakati mgumu hasa wakituma meseji bila kujibiwa kwa wakati. Meseji kujibiwa kwa wakati ni dalili ya kuwa ulie nae anakuelewa au huko sehemu sahihi. Mambo ya “mbona kimya?” Hayapo kwa anaekupenda.

4. MAPENZI NA UMAKINI.

Mapenzi yana ishara fulani ,hasa umakini wake na upendo wa kweli. Wakati wa kuongea, kukumbatiana na hata kubusiana . Sio rahisi, kuanza kumlazimisha mtu ambaye akupendi aongee kwa mahaba utakayo lakini kwa anayekupenda utamuona tu hata kwa ongea yake. Mwanamke akikupenda hata sauti yake itabadilika kwa sababu ya hisia alizo nazo kwako.

5. IMANI NA KUKUUNGA MKONO.

Sio suala la kumuomba Mwanamke akuamini wewe ni suala linalokuja tu bila ya nguvu au ushawishi wowote. Mwanamke atakuwa pembeni yako tu kwa kila jambo kwasababu yeye anajua fika nawe ni sehemu yake. Masuala ya kumbebeleza Mwanamke akuamini au akuunge mkono,haya ni dalili kuwa bado hajawa wako.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

See also  TAARIFA ZA UONGO WALIZO NAZO WANAWAKE KUHUSU WANAUME.

Related Posts 📫

Yul Edochie speaks out again, throws shade...
CELEBRITIES Popular actor, Yul Edochie brags after being criticized for...
Read more
SERIKALI KUJA NA CHANZO KIPYA CHA MAPATO...
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali iko mbioni...
Read more
WILLIAM RUTO KAMA MAGUFULI ...
HABARI KUU Rais wa Kenya 🇰🇪 Dkt. William Ruto amesema...
Read more
MANENO 5 AMBAYO YANASHAWISHI KILA MWANAMKE KUINGIA...
MAPENZI Kuwepo kwa mitandao ya kijamii kumesaidia na pia kuharibu...
Read more
7 REASONS WHY MEN ALWAYS ASK FOR...
LOVE TIPS ❤ 7 REASONS WHY MEN WILL ALWAYS ASK...
Read more

Leave a Reply