MAPENZI
Siku zote,mwanaume anahitaji kupata heshima na anapoona anapata hicho kitu basi mwenye furaha mno kuliko kawaida, jambo hili umpa motisha na ujasiri wa kufanya mambo mengi mazuri kwaajili yako kama mke na familia yenu kwa ujumla.
MAMBO YENYEWE NI HAYA.
1. Wewe ni mwanaume bora kwaajili yangu
2. Kukubali au kukupa nafasi wewe ulikuwa ni uamuzi sahihi kwangu
3. Mimi na watoto wetu hatuwezi kukushukru inavyostahili kwa jinsi unavyotupenda kama familia yako.
4. Wewe ni baba bora na mtu wa kuigwa
5. Sitokaa niwe na mtu mwingine zaidi yako
6. Unanifanya niwe na tabasamu ambalo hakuna wa kunipa zaidi yako
7. Tuwe kwenye nyakati bora za maisha au nyakati mbaya mimi nitakuwa nawe mume wangu
8. Daima nitakuwa upande wako mpenzi
9. Ninapenda kila kitu kutoka kwako
10. Nimekuwa mwenye bahati kupata baba mlezi wa watoto wangu.
Kila mwanaume akipata maneno haya,atajiona bora na atawekeza zaidi kwako na familia kwa ujumla.