MAPENZI
Watu wengi sio vijana au mabinti pekee ni wenye uhitaji wa kuwa na wenza hata walioachika wana uhitaji wa kupata wenza wao.
Ukiwa ni mwaka mpya ,sasa unatakiwa kukaa kwenye maeneo sahihi ili uwezeke kupata mwenza wako. Sasa hapa kuna mambo fulani ya kuzingatia ili uonekane,upatikane na uweze kupendwa. Fanya yafuatayo;-
HAKIKISHA UNAKUWA WA KUONEKANA NA KUPATIKANA
Baadhi ya vijana na mabinti muda mwingi wanajificha hali inayopelekea kutoonekana au kupatikana. Anayetaka kuoa au kuolewa hayuko pekee hapo kanisani kwako au kazini kwako,ebu toka na tembea maeneo mengine kama Beach, Masoko,Shughuli nk
2. KUWA MTU MWEMA.
Kwenye sehemu yako ya kazini au Msikitini au Kanisani, jitahidi uwe ni mtu unayeongelewa vizuri. Fanya kazi kwa bidii na jitume ,kwa kufanya hivi huwa unatengeneza mahusiano ya kupata mwenza. Kanisani, ni nani binti hapendi kuolewa na kiongozi wa kwaya au kijana mtoa zaka mzuri?
3. JIPENDE NA JIKUBALI.
Hakuna wa kukupenda zaidi yako kama sio wewe. Vaa vizuri, kula vizuri, fanya mazoezi kwa ajili ya afya na mambo kama hayo.
4. TUNZA AFYA YAKO.
Afya nzuri ni mtaji mkubwa sio kwa binadamu pekee hata wanyama wa porini. Mfano, porini Simba akiumwa wenzake huwa wanamtenga kwasababu wanajua hawezi kuwinda tena. Kwa binadamu, kijana au binti ukiwa na magonjwa kama UKIMWI Tayari unakuwa unapoteza mvuto.
5. KUWA MWENYE SURA YA TABASAMU .
Sura ya kung’ara inatia matumaini hata kama huna hela.
6. KUWA MNYENYEKEVU NA MWENYE HESHIMA.
7. KUWA MTU WA KUAMINIKA.
Uaminifu ni mtaji. Jifunze kuwa muaminifu hata kwenye mambo madogo na hata makubwa.
8. JIPE THAMANI.
Usiwe tu mtu wa kawaida, jikuze katika elimu na hata kazi yako. Kama ulikuwa huna hela,zitafute mpaka uzipate.
9. KUWA MTU WA KUSAMEHE.
Watu wengi wamekosa wenza kwasababu ya kutokuwa na msamaha . Jifunze kusamehe kwasababu ndoa inahitaji msamaha sana.
10. USIWE MTU USIYEINGILIKA.
Ogopa sana watu kukuongelea kuwa wewe sio mtu wa watu. Kuna wasichana wanaona wao hawapaswi kuongea na baadhi ya watu au ni wabaguzi kwa baadhi ya watu . Usitengeneze mazingira ya kuogopwa kwani wewe ni nani usitongozwe?
Najua malengo ya mwanaume au Mwanamke ni kuolewa kwahiyo tengeneza mazingira ya kuolewa na usijiweke wa gharama au thamani kuliko watu wengine.