MAPENZI.
Kila Mwanamke ambaye anaipenda Ndoa yake,jambo la kwanza la kufanya ni kujifunza tabia za mwanaume wake .
HIZI NDIZO TABIA ZA WANAUME
1. Kila mwanaume ( awe ni mtoto) ana hisia za utambuzi wa kutokuheshimiwa au kudharaulika kwenye kila maongezi yako kama Mwanamke.
2. Mwanaume anapenda heshima kuliko chakula. Fanya yote lakini usimpe mwanaume nafasi ya kutambua kuwa kadharaulika.
3. Wanaume hawapendi majibizano yaani wakiongea nawe uongee. Mwanaume hapendi kuongea nawe halafu nawe humsikilizi unaendelea na mambo.
4. Wanaume huchukia kutishwa na wanawake. Kumtisha mwanaume, haina mbolea kwako Mwanamke.
5.Kila mwanaume anapenda kufarijiwa. Mwanaume yuko tayari hata kuchepuka akikosa faraja ndani ya moyo wake. Wengine, wametelekeza mpaka familia kwa kufuata faraja ya moyo kwa wanawake wengine ambao tu ni wa kawaida.
6. Mwanaume anapolaumu kwa jambo fulani tambua anakuwa amefika mwisho wa uvumilivu. Msaada wako kama Mwanamke ni kutatua jambo hilo haraka iwezekanavyo.
7. Mwanaume anapoongea na wewe huwa anahitaji ukae kimya na kumsikiliza yeye. Ukimya wako unaweza kumfanya ashushe sauti yake kama alikuwa anaongea kwa jaziba.
8. Ukimya wa mwanamke huwa unamtisha mwanaume mpaka huwa anajitahidi kutafuta sababu ya ukimya huo.
9. Hakuna mwanaume mwenye kazi nyingi (busy) kwa Mwanamke anayempenda.
10. Kila mwanaume huwa anahitaji faraja baada ya kazi zake. Mpe chakula na pia mwandalie maji aoge ajihisi yuko sehemu rafiki na salama.
11. Kila mwanaume anapompelekea zawadi mke wake ni kwamba huwa anatafakari sana kabla ya Kufanya hivyo.
12. Kila mwanaume huwa ana kawaida ya kutembea na mawazo ya kile anachokifanya . Mfano kama ni biashara, ukiwa nae kwenye maongezi huenda akawa ana mawazo ya kukuza biashara yake hiyo.
13. Wanaume wanapenda ngono . Wanawake wanapenda kufanya mapenzi.
14. Wanaume wana kawaida ya kubembeleza iwe kwa uongo au ukweli kwa malengo fulani.
15. Kila mwanaume ana nguvu ya kumpiga Mwanamke, sema wengi wameamua kuitumia nguvu yao kuwalinda wake zao.
16. Kila mwanaume anayepata faraja nyumbani mwake daima huwa anarudi kwake mapema.
17. Kutafuta kumtawala mwanaume au kumuweka chini yako ni sawa na kuweka mji kwenye nyumba yako.
18. Mwanaume huwa ni wa pili kuamua kubadili dini lakini kwa Mwanamke ni jambo la kwanza.
19. Hakuna jambo linampa nguvu mwanaume kama kupongezwa na mke wake.
20. Hakuna mwanaume mwenye masihala kwa mkewe mbele ya watoto wake endapo mke wake huficha mapungufu yake.