MAPENZI
Nyumba nyingi zina vilio, mateso ,maumivu na hata visasi ni kwasababu tu wanawake katika nyumba hizo hakuna anaewajali. Wanaume wengi wanakosea. Mwanamke anapokuwa na furaha basi hata mambo ya mwanaume yanaenda vizuri. Soma zaidi
1. Mpende mkeo na mfanye kuwa Malkia naye atakufanya Mfalme. Biblia inasema ” Ibrahim alimpenda Sarah,mpaka Sarah akamuita Bwana wake”.
2. Mfanye kuwa mke bora mpaka awe kama roho Mtakatifu na sio pepo kwako.
3. Msahihishe kiupole mkeo sio kwa kumpigiza makelele
4. Usimlinganishe mkeo na wanawake au Mwanamke awaye yote. Mkeo ni wa pekee Duniani, hakuna kama yeye.
5. Mpe zawadi mbalimbali hasa kwenye matukio yake muhimu kama siku ya kuzaliwa nk na pia jenga mazoea ya kuwa mnatoka wote na kutembea pamoja.
6. Mhudumie mkeo kwa Kadri unavyojaliwa. Baadhi ya wanaume, hujali wanawake wa nje kuliko wanao ishi nao. Kiukweli wako kinyume na kisemwacho kuwa “Ibada njema inaanzia nyumbani “.
7. Jali familia ya kwao na mkeo. Usijaribu kuwafanya ndugu wa mkeo maadui, wawe ni marafiki zako.
8. Mpongeze anapokuwa amefanya jambo
9. Daima ,mfanye mkeo ajue unampenda hasa kwa vitendo.
10. Mpe muda mzuri wa kuwa nawe,mpe muda wa kuzungumza nae na msikilize mpaka aone kweli yuko sehemu sahihi au Mbingu ndogo. Mpe muda mpaka aone kwamba hakuna mwanaume mwingine zaidi yako.
Mwanzilishi wa Ndoa ni Mungu mwenyewe lakini pia kampa mwanaume mamlaka juu ya Ndoa. Mjenzi wa kwanza wa ndoa ni mwanaume, kwahiyo basi ukihitaji ndoa yako iwe nzuri kwa kila mtu ,wekeza kwa mkeo kwanza.