MAPENZI
Kwenye Dunia ya leo,tamaa ya wanawake wengi ni kuwatawala wanaume katika mambo mengi .
Sasa haya ndiyo mambo ya kufanya ili kumtawala mwanaume
1. Muite kwa majina ya mahaba
2. Mpe nafasi ya kuwa kichwa cha familia
3. Usimkwaze zaidi hasa anapokuwa kachukia
4. Kuwa mkimya anapokuwa na hasira. Nenda kipindi ambacho yeye katulia na mweleze ni kwanini ulimkasirisha?
5. Fanya haraka kuomba msamaha hasa unapogundua umekosea. Jitahidi kumkumbusha msamaha na ikiwezekana mfuate na umbusu kidogo.
6. Mwongelee vizuri mumeo kwa watoto na hata marafiki zake.
7. Mheshimu mama yake / mkweo
8. Mkazanie awe anawanunulia zawadi wazazi wake sawa nawe unavyofanya kwa wazazi wako.
9. Ikitokea mumeo hana hela ya kununulia mahitaji ya ndani,nunua wewe.
10. Epuka dada wa kazi kumwandalia mumeo chakula na wewe upo. Wanaume wana akili ya kipekee yaani dada wa kazi anaweza kuwa mke mwenzako.
11. Jenga mazoea ya kumkumbatia mume wako pale anapotoka kazini na pia mpokee alichobeba kama kipo.
12. Mpe tabasamu mumeo
13. Msifie mumeo mbele ya watoto wenu ikiwezekana.
14. Muogeshe mumeo . Jitihada uwe unamsugua mgongoni.
15. Weka kitu chochote cha kuashiria upendo kwenye mfuko wa koti,suruali au kwenye mkoba wake. Weka labda karatasi yenye maandishi ya kumtakia heri nk
16. Mpigie simu au tuma ujumbe kwamba unamkumbuka na unampenda.
17. Ukimpigia simu kabla ya yote mwambie “Nakupenda mpenzi au mume wangu”.
18. Kama umeolewa na mtu maarufu, hakikisha unamfanyia mpenzi wako kila aina ya mapenzi ili akiwa kazini asahau hisia kwa wanawake wengine.
19. Mwambie ulivyo na bahati kuolewa na yeye.
20. Mkumbatie mumeo bila ya yeye kutegemea
21. Mshukuru MUNGU kwasababu huyo ni Adam wa maisha yako.
22. Daima muombee mumeo
23. Omba na mumeo kila siku asubuhi na usiku.