MAPENZI
Kuna mambo mengi ambayo wanaume wengi wangependa kufanyiwa na wake zao,lakini huwa sio majasiri wa kuyasema.
Wanaume huwa hawapendi kuonekana wanapenda sana au kuonyesha ushawishi kwa wapendwa wao,huwa wanakaa kimya.
Lakini ukweli ni kwamba wanaume wanataka mambo haya:-
1. WANAPENDA KUPENDWA.
Wanawake huwa wanapenda kupendwa lakini hiyo haiishii kwao pekee hata wanaume wako hivyo pia .
Wanaume ujiona wenye thamani mno wanapopata kujua kwamba nao wanapendwa.
2. KUHESHIMIWA.
Wanaume huwa wanatafsiri heshima kama upendo wa dhati . Kila mwanaume anataka kuheshimiwa na mke wake hasa. Heshima huwa unamvutia sana mwanaume lakini ikitokea akagundua ,mke wake hana heshima basi mapenzi huwa yanashuka.
Mwanamke kuwa makini sana kwa ili hasa pale marafiki au ndugu wa mumeo wanapokuwepo.
3. KUPONGEZWA NA KUSIFIWA.
Kila mwanaume anapenda sifa hasa za mke wake kama kumwambia yeye ni mzuri,anajua mapenzi, ana upendo au anajali.
Mwanaume angependa sifa hizi lakini hawezi kukwambia.
4. URAFIKI.
Kila mwanaume anapenda kuwa karibu muda mwingi na mtu anayempenda. Kubadilishana mawazo na mtu anayependa ni jambo ambalo wanaume wengi wanalipenda.
Hata kama ikitokea mwanaume hajui mahaba lakini angependa urafiki na mke wake.
5. MWONEKANO MZURI.
Wanaume nao hawako mbali na kuonekana wenye mvuto ingawa ni jambo ambalo huwa wanalificha kwa wake zao. Ni nadra sana ,mwanaume kumuuliza mke wake kuhusu mwonekano. Pamoja na kuwa ni jambo la siri lakini Wanaume wangependa kuwa na mpangilio mzuri wa kuvaa na hata kunyoa nywele na ndevu.
6. KUPEWA HAMASA NA KUAMINIWA.
Kila mwanaume anapenda Mwanamke wa kumtia moyo na kumwamini vilevile na sio wa kumkatisha tamaa.
7. KUTHAMINIWA.
Kwenye kila jambo ,liwe kubwa au dogo mwanaume huwa anapenda kuonesha ushujaa wake. Ingawa ni vigumu kuomba thamani hiyo lakini wanaume wanatekwa sana na Mwanamke ambaye hata kwa mambo madogo anaona thamani.