MAMBO 17 AMBAYO YANAWEZA KUSABABISHA UKOSE RAHA YA TENDO LA NDOA

0:00

MAPENZI

Kwa wanandoa walio wengi ili ni mojawapo ya janga. Sasa leo tuone sababu hizi na hapo kama mwanandoa utaamua kutafuta tiba.

1. KUKOSA UPENDO.

Upendo ni kichocheo kikubwa, unapokuwa unapendana na mtu wako,utaona kila kitu kimekaa kimahaba,utakuwa tu mtu wa kuanguka kwenye raha. Mapenzi ni zaidi ya kufikia kwenye kilele, ni suala la kila mwanzo wa mahaba na ni safari ya kukupeleka kwenye kilele ambacho kilele ndio sababu ya mapenzi. Hii ndio sababu unatakiwa kuwa kwenye ndoa na mtu unaempenda.

2. MAWAZO YA KUPITILIZA.

Unapokuwa unafanya mapenzi, punguza mawazo ili uruhusu raha itawale. Weka pembeni shida zako kama gharama za maisha, kulea watoto, majukumu yako ya kikazi yanayokunyima au kukupa riziki. Yote haya,yaweke kando kwani unahitaji raha hii na ndio tiba ya akili yako.

3. MTAZAMO WA KULINGANISHA.

Ukiwa na mtazamo wa kulinganisha kuhusu jinsi ya kufanya mapenzi unakokuona au kusoma kwenye simu au magazeti na uliye nae ni tatizo. Maneno ya marafiki zako unavyosikia wakilisemea jambo hili, maumbile ya mkeo na mambo kama hayo yanaweza kukunyima ladha ya penzi. Acha Ulimwengu useme yake lakini hapo kitandani mnakipiga nyinyi wawili.

4. KUTAZAMA VIDEO ZA NGONO.

Unapokuwa mpenzi wa video hizi basi unatengeneza hatari ya kutembea na mawazo ya video hizo. Utamuona mwenza wako hana analojua kwasababu tayari kuna picha kubwa unayo kwenye akili yako,hata ukifanya mapenzi unakuwa humuoni yeye bali yule uliemuona kwenye video hizo. Video za ngono ni moja ya jambo linalochangia kupunguza hamu ya tendo la ndoa.

5. UASHERATI.

Kulala na watu wengi kunakukausha. Huwezi kuona raha kwa ulie nae kwasababu utataka awe kama fulani uliyewahi kuwa nae na fulani ukiwa nae utaona ana mapungufu sio kama fulani, mwisho wa siku utakosa raha ya ndoa.

6. TUHUMA.

Ukiwa unamtuhumu mpenzi wako kwamba hana uaminifu kwenye Ndoa yenu ni rahisi mwili wako kukosa nguvu hasa unapokuwa nae. Tendo la ndoa linaanzia kwenye fikra zako,mawazo ya kuwa mwenzangu alikuwa wapi au sijui ataniambukiza magonjwa, yanaweza kukunyima nguvu ya kufanya mapenzi.

7. UGOMVI.

Ni vigumu kupata raha kwa mtu ambaye una ugomvi nae ,mtu anayekudharau ,anayekuumiza au kukuchukulia poa. Mapenzi sio kwaajili ya watu wenye migogoro ,kama una mgogoro umalize kabla ya kupanda kitandani . Ugomvi unapoteza ladha ya mapenzi.

8. KUTOKUJIANDAA KWAAJILI YA TENDO .

Je una maandalizi kwaajili ya tendo lenyewe? Je mwenza wako anapenda sehemu zako za siri zilizonyolewa? Je unavaa nguo kwaajili ya tendo hili? Je unafahamu mwenza wako anataka nini kitandani? Kitandani ni mbingu,fanya mbingu yenu na mwenza wako.

9. KURUKARUKA.

Pamoja na kwamba ni jambo la haraka,chukua muda kujifunza mwili wa mwenza wako unapenda nini? Mjaribu mwenza wako maeneo mbalimbali ya mwili wake na uone ni wapi anafurahia zaidi kuliko wewe kulipuka tu kama Volkano na kupoa.

10. KUCHAGUA MWENZA AMBAYE HAMUENDANI.

Suala la faragha linahitaji mtu ambaye pia mnaendana kwa mambo mengi. Endapo mtakutana kwenye ndoa na hamuendani ,mvuto wa mapenzi utakosekana. Kwa mtu ambaye hamuendani hata akiwa ni mzuri ni vigumu kupata nae hisia kwasababu ya machaguo yake yanakuwa tofauti na yako.

11. MAUMIVU ULIYOWAHI KUPITIA.

Kama umewahi kupitia manyanyaso ya kingono kama kubakwa hata pale utakapokuwa na mwenza wako bado utakuwa na woga . Vilevile hata kama umewahi kufanya biashara za ukahaba ni ngumu ngumu kuja kulizishwa kimapenzi na mwenza wako.

12. USTAHIMILIVU.

Kufanya mapenzi sio jambo la binafsi, ni jambo ambalo linahitaji uimara wako ili nawe uweze kumpa mwenza wako raha. Unapofanya tendo ili jiweke vizuri na uvumilivu unahitajika ili kumpa mwenza wako raha au mwenza wako kukupa raha.

13. SABABU ZA KIAFYA.

Kuna wakati mwenza wako akawa na harufu ambayo sio ya kawaida labda fangasi za miguu zinasababisha harufu kali au hata kunuka mdomo au kwapani. Pia, wanawake wengine wana maji mengi wakati wa kujamiana jambo ambalo huwa linawafanya wenza wao kuoga mara kwa mara wawapo kwenye tendo ilo. Ubaya wa ili upo endapo mwenza wako atakueleza tatizo lako kwani litakunyima kujiamini.

14. KUKOSA UBUNIFU.

Kurudia rudia mtindo uleule wa kufanya mapenzi ni jambo ambalo linaweza kukunyima hamu au kumnyima hamu mwenzako mnapokutana kimwili.

15. KUFANYA TENDO LA NDOA KAMA WAJIBU.

Tendo ili linapaswa kufanyika kama mapenzi na sio wajibu. Jambo la hatari ni pale unapofanya tendo ili na mwenza wako kama tu kutimiza matakwa ya ndoa. Kufanya mapenzi sio jambo la upande mmoja,kwamba mwenzako akijisikia ndio mnafanya. Wanawake wengi wamekuwa wakifanya jambo ili sana ndio maana wengine wamefika hatua ya kukata tamaa kwasababu wao mpaka mwanaume aanze.

16. KUONA TENDO LA NDOA NI DHAMBI.

Kwenye jamii zetu,kwa jinsi tulivyokuzwa na kulelewa suala la kujamiana huwa linaonekana ni dhambi kubwa. Wachungaji,Makanisani wanafundisha na kututia woga juu ya jambo hili . Kwenye mazingira kama haya ni vigumu kuendelea kumshawishi mtu mwenye mtazamo hasi wa tendo ili. Lakini Kwenye ndoa ni mahali sahihi pa kusema uchafu wowote bila kificho kuhusu tendo ili la mapenzi.

17. WOGA WA UJAUZITO.

Hata waliopo kwenye ndoa ,huenda wakawa na wasiwasi na jambo ili kwasababu kila mzazi anapenda akileta kiumbe basi awe na uwezo wa kukihudumia kwa ubora. Kufanya mapenzi kwa wasiwasi kuna shusha hari na hamu ya tendo ili kwasababu, woga huwa unaamisha hisia. Ni vyema basi kuwasiliana na Daktari akupe taarifa zaidi kuhusu uzazi salama ili uendelee kupata raha ya tendo ili.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

YANGA YAINGIA MKATABA WA MILIONI 300 ...
MICHEZO Klabu ya Yanga imeingia Mkataba wenye thamani ya Tsh...
Read more
“ REASONS WHY SOME WOMEN ARE NOT...
SHYNESSMost women are shy to the extent of finding it...
Read more
GEREMI NJITAP AKUBWA NA MKASA MZITO
NYOTA WETU Ndoa ya Nyota wa zamani wa Chelsea na...
Read more
The wife of the former Presidential candidate...
POLITICS Maryanne Moghalu, wife of the 2019 Young Progressive Party...
Read more
What is Right Courtship
We all know what it is, right? If you don’t,...
Read more

Leave a Reply