MAPENZI
Huenda kuna sababu zilizo nje ya uwezo wako lakini hizi ndizo sababu zilizo ndani ya uwezo wako ambazo zinakufanya usiwe mke au mme wa fulani:-
1. Huwa unawaona watu tofauti na walivyo
2. Unafanya maamuzi kwasababu ya kuhitaji mtu wa kukuondolea upweke tu
3. Huna uhakika kipi unahitaji kwenye mahusiano yako
4. Hauoni thamani yako na hujui thamani yako ni ipi?
5. Unataka kubadili kila kitu kwa mwenzi wako
6. Ni mtu mwenye mipango mingi lakini huitimizi au ni mtu wa maneno mengi matendo sufuri.
7. Ni mtu ambaye huna ujuzi au uwezo wa kuwasilisha hisia zako kwa mtu bila kumkwaza
8. Unaamini unaweza kuishi pekee yako na ukawa na furaha
9. Ni mtu ambaye unaishi maisha yasiyo yako
10. Ni mtu muoga kitu ambacho kinakufanya uwe mtu wa chini
11. Ni mtu mwenye bidii ya kujibadili usiwe wewe. Jikubali kuwa ni wewe.
12. Ni mtu wa kuruka ruka . Tulia na tengeneza njia nzuri ya mahusiano
13. Ni mtu ambaye uombi ushauri kwa watu wengine.
14. Ni mtu ambaye unapenda kuwekeza muda kwa yaliyopita. Mfano kuendelea kumtafuta “ex” wako.
15. Ni mtu usiyeona jambo jema kwa walioko kwenye Ndoa.
Ukipata mtu ambaye sio sahihi kwako usiwe mwisho wako kupenda kwani hayo ni makosa ambayo yapo lakini pia mtu sahihi kwaajili yako yupo.