MAPENZI
Uamuzi wa kuoa na kuolewa unahitaji kutafakari kwa kina kama ambavyo ,wengi huwa tunampokea Kiristo kuwa Bwana na Mwokozi wetu .
Unaemuoa au kuolewa nae ana athari kwaajili ya maisha yako ,kwahiyo uamuzi wa kumchagua mwenza wako unatakiwa uwe sahihi.
MAMBO YA KUZINGATIA ILI UFANYE UCHAGUZI SAHIHI.
1. ELEWA NIA YAKO.
Kwanini upo Duniani? Kabla ya kuchagua mwenza ni bora kufahamu malengo ya MUNGU kukuleta Duniani ili iwe rahisi sasa kupata mtu unayeendana naye. Malengo ya Ndoa ni kutimiza makusudi ya MUNGU pia,kwahiyo ukiwa na mtu sahihi ni rahisi. Kuna watu wengi wameshindwa kutimiza makusudi ya MUNGU kutokana na wenza walio nao.
2. JIPENDE.
Wewe ni wa thamani, kipekee na maalumu. Ni vema kutambua hivi vitu ili isionekane kuoa au kuolewa kwako ndio kumekupa kibali cha hayo yote. Jikubali kwa jinsi ulivyo. Ione sehemu ambayo ni bora kwako na sehemu iliyokuwa na mapungufu iwe ya kuiboresha zaidi. Jinsi unavyojiona bora basi huwa inakuongezea kujiamini zaidi na kukuondolea woga . Kujipenda kwako ni tangazo tosha hata kwa mwenza wako ajaye kwamba wewe huko hivyo.
3. UKOMAVU.
Ndoa inahitaji Mwanamke na Mwanaume sio Msichana au Mvulana . Unahitaji mtu mwenye ukomavu wa kiroho,kiuchumi, kihisia na kimwonekano kabla ya kufanya uamuzi wa kuchagua mwenza wako wa maisha.
4. PATA USHAURI .
Kabla ya kuchagua mwenza wako wa maisha ni vizuri kupata ushauri kutoka kwa watu wengine, ushauri ambao utakufungua kuhusu mapenzi maana mapenzi ni upofu. Ukiingia tayari kwenye ndoa sio rahisi kusikiliza ushauri kwasababu mapenzi yana kawaida ya kufunga kitambaa cheusi machoni.
5. HISTORIA.
Ni muhimu kuangalia mwenza wako ametokea kwenye mazingira ,lugha,mila na desturi, na hata familia. Ukiwa na historia ya mwenza wako basi itakupa uelewa mpana hata wa kuishi nae vizuri.
6. UPIMAJI WA AFYA.
Kabla ya kumchagua mwenza wako wa maisha, suala la afya ni muhimu. Upimaji wa magonjwa, aina ya damu nayo uamua mpenzi wako kwenye kuishi vizuri hata kifamilia.
7. PIMA UPENDO.
Mwenza wako wa maisha ni vyema kumpima kama ana upendo ambao MUNGU mwenyewe anauagiza. Upendo ambao hauna masharti maalumu.
8. PIMA AMANI YAKO.
Mshirikishe MUNGU kwenye jambo ili kwasababu ukiingia kwenye agano la ndoa na mtu ambaye huna amani nae ni jambo ambalo linaweza kukupa wakati mgumu kwenye maisha. Mtangulize MUNGU mbele aliye chanzo cha amani na pia akupe mtu wa kukupa amani ya moyo.
9. CHAGUA MTU MNAYEENDANA.
Ni vigumu kupata mtu ambaye mnaendana kwa mambo yote lakini mtu ambaye mnaendana kwa mambo mengi ndiye mtu sahihi. Mambo kama ya kiimani,malezi ya watoto na mambo kama hayo ni vizuri muwe mnaendana.
10. UWE NA TABIA ZA KIUNGU.
Mungu ni upendo, kwahiyo ukiwa na sifa na tabia zinazoendana na MUNGU basi utakuwa huko sawa kabisa kuishi na mwenza wako.