MAPENZI
Duniani hakuna mkamilifu wala ukamilifu ingawa kila siku tunautafuta ukamilifu huo.
Lakini kwenye mahusiano kuna mapungufu ambayo hutakiwi kuyaonyesha ukiwa kama sehemu ya mahusiano hayo ni kama :-
1. EPUKA KUWA CHANZO CHA MIGOGORO.
Kuna watu huwa wanaanzisha migogoro ambayo hupelekea wao kuachika na hufikia hali ya kukata tamaa na kuona ,huenda mahusiano ni jambo baya ilihali wao ndio chanzo cha mgogoro.
2. KUTAKA USHINDANI.
Kuna jambo likianzishwa basi kati yenu kuna mmoja anataka tu yeye ashinde mazungumzo au asikilizwe yeye pekee. Kwenye mazingira ya mahusiano, huwa hatutafuti mshindi wa hoja bali maelewano.
3. USITAKE KUONEKANA WEWE NDIO MWENYE UPENDO.
Mahusiano yanajengwa na watu wawili,kila mtu kuna anavyotamani mwenzake amfanyie ila sio kweli kila siku uwe ni wewe pekee.
4. ACHANA NA MASUALA YA KUTAKA KILA MTU AWAZE KAMA WEWE.
Kila mtu akitimiza majukumu yake,sio lazima kila mtu awaze kama wewe kwa kila jambo. Inaweza kuwa hivyo,lakini hakuna ulazima.
5. ACHA BIASHARA YA MTU KUKUSOMA AKILI ZAKO.
Mtu anaweza kutimiza matakwa yako endapo utamwambia ila ukikaa kimya na kusubiri kuwa akusome unachowaza,hiyo ni MUNGU pekee anaweza kusoma akili na mawazo ya binadamu.
6. ACHA KUWEKA MIPANGO YAKO YOTE KWA MTU MMOJA.
Hakuna mtu ambaye atakufanyia kila kitu . Kikubwa ni kuwa karibu na watu mbalimbali kama marafiki, ndugu na jamaa. Hata upate tajiri yupi,haiwezi kuwa kama unavyotaka.
7. USILAZIMISHE USICHOPENDA WEWE NA MWENZAKO ASIKIPENDE.
Mahusiano yana mipaka, sawa lakini kila mtu ana mipaka yake na kwasababu na wewe utakuwa na mipaka yako na kwasababu basi usimlazimishe mwenzako awe na mipaka kama yako.
0