MAPENZI
Hapa kuna ugumu hasa suala la mahusiano ya kawaida na upendo! Uelewa wa kwanini mwanaume anampenda Mwanamke ni mchanganyiko wa hisia na sababu za vitendo na ndivyo uleta mvuto pia.
Haya ni mambo ya msingi ambayo mwanaume anavutwa nayo kumpenda Mwanamke
1. UHALISIA.
Kuwa mkarimu,muwazi, na mwenye heshima kwa watu ni moja ya alama ya mtu anayeweza kutengeneza mahusiano imara. Wanaume ni wajenzi wa mahusiano, wanapenda Mwanamke halisi.
2. KUSAIDIWA.
Wanaume huwa wanathamini mchango mkubwa wa Mwanamke hasa aliempa msaada kwenye mapito yake au aliyemfanya kufikia malengo. Kuwa na mtu anayeweza kuhimili vishindo vya majaribu na kusonga kuifikia nchi ya ahadi.
3. MUUNGANO WA KIHISIA.
Mwelewa wa hisia,mwenye kujua thamani, mwenye kutamanika,na mwenye upendo unaovuka mipaka mpaka kuzaliwa mvuto. Kuwa pamoja kwa muda mrefu pia hujenga ukaribu na urafiki.
4. MWONEKANO.
Sura ina mchango mkubwa lakini pia wanaume huvutiwa na tabia. Tabasamu, uvaaji mzuri na pia mvuto wa macho ni vivutio vizuri kwa mwanaume.
5. VIWANGO.
Mwanamke mwenye akili, huruma, wema, uaminifu ni kiwango au tija ambayo mwanaume anaitaka.
6. MAONO.
Wanaume wanavutiwa na Mwanamke mwenye maono ya mbali,watahitaji kuweka nguvu ili kumpata. Mwanamke mwenye akili ya maisha ni lulu kwa mwanaume.
7. MWENYE KUJITEGEMEA.
Wakati mwingine mwanaume anaweza kumpenda Mwanamke mwenye mipango yake akaona nae anamfaa. Kusaidizana kwenye kutimiza ndoto ya kila mmoja nayo ni mchakato wa kuwa na mahusiano mazuri pia.