MAPENZI.
1. Wanawake wengi huwa wanavaa ili kuonesha uzuri wao kwa watu wa nje Zaidi kuliko wanavyovaa mbele za Wanaume wao wa ndoa wakiwa ndani. Wewe,Mwanamke mtazamaji wa kwanza ni mumeo.
2. Wanawake wengi huwa wanalalamika ya kuwa waume zao hawawaridhishi kwenye suala la tendo la ndoa lakini hao wanawake hawataki kusema ,wapeweje haki yao hiyo ya kindoa. Wewe Mwanamke, mumeo sio mtabiri,funguka.
3. Wanawake wengi wana aibu kitandani, kwasababu hawajiamini jambo hili huwafanya wanaume wengi kuhisi kama wanawalazimisha kuwaingilia kimwili. Wanawake jitahidini kujiamini ili kufanya suala la faragha kuwa zuri.
4. Wanawake wengi huwa hawapendi kutoa sifa kwa waume zao hasa wanapokuwa kitandani. Mpe sifa zake mumeo anapokugusa mwili wako nk. Mpe mumeo kujiamini.
5. Wanawake wengi hupenda kuwadogosha waume zao kwa kuwafokea. Jambo hili linaharibu ladha ya mapenzi. Wakati wa tendo la ndoa sio muda sahihi wa kumkumbusha mumeo juu ya mshahara wake ulivyo mdogo na hata kejeli nyingine.
6. Wanawake wengi kitandani huwa hawana habari ya kuanzisha mchezo. Wengi ndio kwanza ujifacha wanaumwa au kuleta sababu ili tu basi wasishiriki kwenye mchezo huo. Wanawake, hata wanaume wanapenda kushirikiana nanyi kwa kupeana ushauri kabla ya tendo.
7. Wanawake wengi huwa wanahisi kuwasema vibaya na kuwalaumu waume zao ndivyo inawastahili waume. Mwanaume anahitaji kusikia maneno ya faraja, tabasamu lako na hata kutiwa moyo. Mwanaume anayesemwa vibaya, anakosa ubunifu kwenye tendo na hata kupoteza mvuto kwenye tendo.
8. Wanawake wengi huwa wanalalamika kuwa wanaume wao wanapenda tendo la ndoa sana. Hata pale mwanaume anapoacha kuzungumza habari hizo,Mwanamke bado huwa analalamika akidhani mwanaume bado anataka tendo.
9. Wanawake wengi hutumia tendo la ndoa kama silaha. Wakati wa mazungumzo, huwa wanakaa kimya ili baadae wakatae kushiriki kwenye suala lenyewe. Baada ya muda mwanaume huwa anaamua nae kukaa kimya,Mwanamke akirudi ili kuendeleza mapenzi tayari Ufa huwa tayari umetokea.
10. Wanawake wengi huwa hawajali kuhusu afya ya mwili kiujumla. Wengi hukosa muda wa kuoga hasa kuosha sehemu zao za siri,jambo hili huchangia pakubwa wanaume wengi kutojihusisha kwenye tendo la ndoa.
11. Wanawake wengi hasa walioishika dini wana amini tendo la ndoa ni uchafu hata kama wameolewa. Wengi wanaamini tendo hili ni takatifu na ni lazima walitoe tu kwa wanavyojisikia wao. Wanawake ,kama nawe ni mshika dini tambua ,MUNGU amekupa mwili huo kwaajili ya mwenza wako vilevile.
12. Wanawake wengi ni waoga wa tendo hili. Nawe kama ni miongoni mwao,kuwa huru acha mwili ufanye mambo yake.
13. Wanawake wengi wana kawaida ya kufananisha penzi la zamani yaani kwa mtu aliyewahi kuwa nae na anataka afanyiwe kama yule lakini ukweli ni kwamba kila zama na mbuyu wake.