NYOTA WETU.
Mohamed Ramadan kutoka nchini Misri ndiye anatajwa kuingiza hela ndefu na ni miongoni mwa wasanii wa Afrika wenye mafanikio.
Mohamed (35) mzaliwa wa Qena inatajwa alilipwa dola milioni 2.5 (bilioni 6.3) kushiriki kwenye Tamthilia ya “moussa” mwaka 2021, na dola laki 927 (bil 2.4) kushiriki kwenye Tamthilia ya “The Prince ” mwaka 2020.
Mwimbaji huyo wa Ya Habib ana jumla ya wafuasi milioni 29 Instagram, milioni 23 Facebook.,subscribers 15.3 youtube, Tiktok 8.5 milioni na kwenye mtandao wa X ana 2.9 milioni. Jumla ya wafuasi wake kwenye mitandao ya kijamii ni 78.7 milioni.
Ramadan alishiriki kwenye soundtrack ya AFRICON 2023 “Akwaba” akiwa na Yemi Alade na Magic system ambao walitumbuiza kwenye ufunguzi wa michuano ya AFRICON.