MAPENZI
1. Vaa nguo laini ambayo ni nyepesi kuivua na inayokupa mvuto kwa mwenza wako. Ifanye iwe rahisi kwa mwenza wako kuweza kuyafikia maeneo nyeti . Kwa matokeo mazuri ya kuondoa usumbufu, lala mtupu.
2. Piga mswaki kabla ya kulala ili uwe na mdomo wa kuvutia.
3. Usiingie kitandani na kazi zako nyingine
4. Achana na matumizi ya simu au computer. Mpenzi wako anahitaji utulivu wako.
5. Waamishe watoto kwenye chumba kingine kama uwezo upo. Kitandani ni sehemu sahihi ya kutengeneza uzao mpya.
6. Wanaume hupata hisia za haraka wanapobusiwa usoni,mdomoni au kushikwa kifuani nyakati za usiku. Fanya hivyo Kadri uwezavyo ili kumvuta kwenye Ulimwengu huo mpya.
7. Usiku ni muda mzuri wa kupeana sifa nzuri . Msifie mwenzako, kwamba ana umbo au maumbile mazuri. Maongezi kitandani ni mazuri mno.
8. Salini pamoja wakati wa kulala na wa kuamka.
9. Msamehe au omba msamaha kwa mwenzako kama amekukwaza mchana. Sio afya,kwa wanandoa kulala na vinyongo.
10. Jifunze lugha ya mwili ya mpenzi wako. Wakati anakuhitaji muelewe na Wakati ambao hakuhitaji na pia haijalishi ni wakati upi?
11. Kuweni na mazungumzo ya kifaragha. Mweleze kuwa amekufanyia vizuri, amekosea au kakuvunja moyo.. Hii itamjenga mwenzako na kuboresha zaidi kwa siku nyingine.
12. Inapotokea mwenzako akajamba,cheka kwasababu kujamba hakukwepeki
13. Mfunike mwenza wako pale unapoamka usiku na kukuta amejifunua shuka.
14. Mbusu mwenza wako pale unapotoka haja wakati wa usiku.
15. Inapotokea mwenza wako ameota jambo kwenye ndoto. Omba nae ,maombi ni silaha.
16. Mpe busu wakati wa kulala na kuamka mpenzi wako
17. Kabla ya kuamka ni vizuri kufanya jambo zuri la kimapenzi kwaajili ya mwenza wako hata kama Alarm itakuwa inaita.
18. Tembea na upendo wa mwenza wako hata kama haupo nae kitandani