MSICHANA WA KUOA ANAPIMWA KWA MAMBO HAYA 12

0

0:00

1. AWE ANAJITAMBUA.

Msichana anaejitambua sio mropokaji au msema ovyo ,kwa kila neno analoongea utaiona akili kubwa yenye hekima na busara.

2. MWENYE HISIA NZURI.

Anayeweza kuvumilia mambo hata mambo yakiwa magumu kwake lakini akabaki mwenye furaha.

3. MWENYE UWEZO WA KUTAFUTA.

Msichana makini ni yule anayeona umuhimu wa kuongeza alicho nacho au alichopewa badala ya kutumia tu. Msichana huyu atumii urembo wake kama kitega uchumi cha kujipatia na kutumia tu. Ni yule,akipewa laki anaikuza inakuwa laki mbili.

4. MWENYE KUPENDEKA.

Wasichana wengi wakionyeshwa kupendwa wao huwa hawaonyeshi ushirikiano lakini kwa msichana mwenye viwango akipendwa nae anapendeka moja kwa moja.

5. KWA CHAKULA.

Msichana ambaye ameiva kichwani, kwake jiko ni mahali sahihi pa kuhakikisha anafanya mambo kuwa makubwa. Atapika na atapenda kukupikia kila aina ya mapishi. Na siku zote Mwanamke anayeolewa na kukaa kwenye ndoa ni yule mwenye kujua kupika.

6. UCHESHI.

Sura ya mbuzi haina maana kuwa mcheshi,tania ,cheka na furahi.

7. JINSI ANAVYOOMBA MSAADA.

Msichana akiwa na huitaji ataomba msaada lakini kuna namna nzuri ya kuomba msaada ingawa wengi misaada yao wanaiomba kwa kauli kali au vitisho. Omba kiutu bila kutisha nk.

8. TASWIRA YA MUNGU.

Msichana ambaye ukiwa nae anakusamehe,kukufariji,kukuombea,kukupenda na kukutamkia baraka ni kishawishi tosha kuamini huko karibu na MUNGU.

9. KUJIAMINI.

Msichana huyu ana msimamo thabiti hasa kwenye maamuzi yake .

10. MWENYE UWEZO WA KUTUNZA MAHUSIANO.

Ana marafiki wa kudumu na hata mahusiano yake anayajali mno na hapendi mahusiano yavunjike. Pia, msichana mwenye mahusiano mazuri na familia yake ni mtu sahihi.

11. ANAYEJALI MWILI WAKE.

Msichana ambaye anajua kuvaa vizuri na kwa staha pia anasuka mitindo mizuri ya nywele. Ni msichana mwenye mwonekano mzuri.

12.FUNDI KITANDANI.

Msichana ambaye anajishughulisha kitandani na sio mzigo kwa mwenza wake. Anampa mpenzi wake inavyostahili ,kiufupi hana hulka za kumbania mpenzi wake.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

See also  MWANAUME UKIMFANYIA HAYA MAMBO 7 HAWEZI KUKUACHA

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Don't miss out!
Invalid email address

Leave a Reply

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading