MAPENZI
Kuna maandalizi ya kufanya kabla ya kuingia kwenye ndoa. Maandalizi haya yafanyike kabla ya kuingia kwenye ndoa kabla ya Mambo mengine.
Kumpenda tu mtu isiwe tu kigezo cha kuoana. Kuna mambo mengine huwa yanachagiza au kuendana na upendo.
Mambo yenyewe ya kuyaongelea ni haya:
1. PESA.
Usidharau suala la pesa kwenye ndoa. Kuna ndoa nyingi zinaingia kwenye migogoro kwasababu ya pesa. Kabla ya ndoa,wekeni mezani mjadala wa pesa ikiwezekana kila mmoja wenu ataje vyanzo vya hela na kiasi anachomiliki. Kwenye mjadala kama huu, mtaweza kuelewa na kupanga namna ya kutunza familia au hata idadi ya watoto.
2. KULEA.
Sio kila anayeingia kwenye ndoa ana uwezo wa kusimama kama mzazi au mlezi. Ni vyema kukubaliana na mwenza wako kama kweli nae ana nia ya kuwa mzazi.
3. WAPI PA KUISHI.
Sehemu ya kuishi kwenu kama wapenzi ni sehemu ya kufahamika kwasababu mnapoingia kwenye ndoa mnaanza maisha mapya. Kuna wapenzi, wanapenda karibu na wazazi wao lakini pia kuna wanaopendelea kuishi mbali na kwao.
4. MALENGO YA MAISHA.
Kila mtu ana malengo na ndoto pia. Kabla ya kuoana ni muhimu kila mtu akaweka malengo yake mezani na yajadiliwe . Ndoa nyingi zina migogoro kwasababu ya kila mtu kuwa na malengo na vipaumbele kinyume na mwenza wake.
5. MAMBO YAKO YA ZAMANI.
Ni jambo baya kuingia kwenye ndoa na mambo yako ya zamani ambayo pia yanaweza kuharibu mipango yako ya mbeleni. Kuna watu ,wanaingia kwenye ndoa na bado wana watu wao wa zamani. Ni vizuri kabla ya kuingia kwenye ndoa, kufuta kila kitu na kuanza upya.