MAPENZI
1. UPWEKE.
Mwanamke akimkosa mtu wake kwenye nyakati zake basi huwa anaona kutengwa au kudharaulika.
2. KUTOSIKILIZWA.
Mwanamke anapokosa kusikilizwa basi huwa anajiona asiye na thamani na mpweke. Sababu hii inaweza kumfanya aache mahusiano.
3. KUKOSA ULINZI.
Mwenza anapokuwa na wivu,mwenye matusi au dharau basi Mwanamke huwa anakosa ulinzi.
4. KUKOSA HISIA.
Mwenza wake anapokuwa mbali au hamuonyeshi kujali ,Mwanamke anaweza kudhani hapendwi au kutamanika.
5. KUKOSA KUSAIDIWA.
Mwanamke anapokosa kusaidiwa katika nyakati zake ngumu au kusikilizwa kwenye malengo yake basi Mwanamke anaweza kuona hayuko sehemu sahihi.
6. KUKOSEKANA MABADILIKO.
Mwenza anapokuwa haonyeshi mabadiliko katika mahusiano hasa kama mnywaji wa Pombe,msaliti wa ndoa na mambo mengine basi Mwanamke huwa anakosa hamu ya kuendelea na mahusiano.