MAPENZI
Mapenzi sio mwonekano au kipato bali Mapenzi yako kwenye
1. MAWAZO.
Ukiacha kipato,urembo, dini na elimu ,sehemu nzuri ya kumpata mtu wako sahihi kwenye maisha yako ni namna anavyowaza mambo yake au yenu. Mawazo ya mtu ndio yanatakiwa kuwa kivutio zaidi kuliko mwonekano au kipato chake.
2. AFYA.
Mtaji namba moja kwa kila kiumbe hai ni siha njema. Litakuwa jambo la kutisha kuingia kwenye mahusiano na mtu ambaye unafahamu fika,afya yake ni changamoto.
3. UAMINIFU.
Mpende mpenzi wako sio kwa kipato au urembo wake bali kwa uaminifu katika maisha yake ya kila siku. Dalili au ishara ya mtu asiye mwaminifu ni kusema uongo. Uaminifu unaenda mbali kwenye mapenzi pale mwenza wako akiwa sio mwaminifu anaweza kutembea na ndugu mpaka marafiki zako.
4. MWENYE KUJIAMINI.
Kujiamini ni ishara ya mtu mwenye amani ya moyo. Mtu ambaye ana amani ya moyo ana uwezo mkubwa kwa kufanya mambo yake kwa unyoofu mkubwa.
5. MKARIMU.
Mtu anayejitoa kwako au kwa jamaa zako ana nafasi ya kuwa mtu sahihi kwasababu yuko kwaajili yako. Mtu mkarimu anatawaliwa na upendo wa dhati kutoka ndani ya nafsi yake.
6. UWEZO WA KUPOKEA NA KUTOA UPENDO.
Kwenye mahusiano kuna watu wanapenda, wao wapendwe pekee bila hata ya kuonyesha hisia za upendo kwa watu wao wa karibu. Wamejaa ubinafsi kwa kutamani wao ndio wapewe tu kila kitu lakini wao hawafanyi hivyo kwa wenzao.
7. UWEZO NA UTHABITI.
Kuna mtu mwenye kitu ndani yake hata kama bado hana fedha ,ni mtu sahihi kwasababu kuna muda ukifika kutokana na uwezo na uthabiti wake atazipata.