MICHEZO.
Mshambuliaji wa Taifa stars, Simon Msuva amesema mashindano ya Mataifa ya Afrika (AFRICON) mwaka 2023 yamemsaidia kupata timu mpya baada ya kuachana na timu aliyokuwa akiitumikia kabla ya mashindano hayo.
“Nimetoka kwenye matatizo na ile timu yangu ya JS Kabylie ya Algeria lakini nilijua mimi kabisa siwezi kukosa timu na ndiyo maana huku ninakokwenda ndiyo nitakojiuza ,nitajitangaza ili niweze kupata timu “
Alisema Simon Msuva.
Msuva amesema alikuwa na ofa kutoka vilabu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoka Uturuki, China na Iraq 🇮🇶 lakini ameichagua Al Najima inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Saudia Arabia kwasababu anaifahamu ligi hiyo.
Kuhusu AFRICON amesema ilikuwa ni matamanio kufuzu hatua ya 16 bora ,lakini hawakufanikiwa,hivyo kilichobaki ni kujipanga zaidi kwa mashindano yajayo ili waweze kufanya vizuri.
Tanzania 🇹🇿 imetolewa ikiwa na alama 2 nyuma ya vinara Morocco, DRC na Zambia.
Related Content