MICHEZO
Jurgen Klopp ametangaza kuwa ataondoka Liverpool mwishoni mwa msimu huu wa 2023-24, baada ya kumaliza muda wake wa miaka tisa katika klabu hiyo.
Habari hizo zimeshtua sana wadau wa soka Duniani kutokana na mkataba wake kumalizika mwaka 2026 ,lakini amekiri kwamba ataachana na majukumu yake hayo kwa kile alichosema “anakosa nguvu “. Klopp mwenye umri wa miaka 56 amekuwa Kocha mwenye mafanikio makubwa.
Klopp aliteuliwa Oktoba 2015 na mkataba wake ulitakiwa kumalizika 2026 . Ameshinda ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2019 kabla ya kuiongoza Liverpool kukata ukame wa kutwaa kombe la ligi kuu ya England, mnamo msimu wa 2019-2020 baada ya kupita miaka 30.

Related Content
Related Content
Related News 
Football Australia face a race against time to install a...
Music executive Ubi Franklin has revealed that he’s still in...
Nigerians left in stunned as singer Tiwa Savage shared her...