MAPENZI
Migogoro ni sehemu ya maisha kwa wanandoa au waliopo kwenye mahusiano na mgogoro unakuja kwa ajili ya kujenga au kubomoa mahusiano. Pamoja na mambo mengine, migogoro haitakiwi kuwa sehemu sana ya maisha kwenye ndoa.
Watu wengi wanaoshindwa kutatua changamoto kwenye ndoa au mahusiano huwa wanaishia kupeana talaka au kuishi kwa maumivu. Ukiweza kutatua migogoro inapotokea una uwezekano mkubwa wa kuishi maisha yenye furaha kwenye ndoa au mahusiano yako.
JINSI YA KUTATUA MIGOGORO KWENYE MAHUSIANO
1. WEKEZA KWENYE KUSIKILIZA.
Jambo la kwanza kunapotokea mgogoro ni wewe kusikiliza kwanza badala ya kuanza kujibizana na mwenza wako. Unaposikiliza,utaweza kusikiliza ni wapi mwenza wako amekasirishwa nako . Ni vizuri zaidi kumpa mwenza wako muda aongee hata kama ataongea mambo ya kuumiza ili aweze kutoa sumu zake zote.
2. USILIPIZE KISASI.
Kama tujuavyo,ubaya haulipwi kwa ubaya . Ikitokea ukawa umefanyiwa jambo baya ni muda wa kutulia. Unapojipa muda wa kutulia itakupa utulivu wa akili ili uweze kufanya maamuzi sahihi ya kujenga badala ya kubomoa.
3. EPUKA KUTUMIA MANENO MAKALI.
Ni kweli unataka usikike wewe lakini epuka kutumia maneno ya kukera (matusi) . Kabla ya kutamka maneno ni vizuri kuwa na akiba na kutumia maneno sahihi na ikiwezekana kwenye mgogoro tumia maneno ya wema na kubariki badala ya kulaani na kulaumu.
4. MNYAMAZISHE MWENZA WAKO KWA UPENDO.
Kunapotokea mgogoro sio muda sahihi wa kutafuta ushindi kwa mwenza wako bali ni muda wa kutafuta mnasongaje mbele? Kuna mambo kama haya ya Kumfanya anyamaze haraka kama kumsifia alivyo mzuri,mkumbatie na ikiwezekana mbusu au mkonyeze kwa jicho la mahaba.
5. OMBA MSAMAHA UNAPOKUWA UMEKOSEA.
Kiburi ni muuaji mzuri wa mahusiano mazuri. Ikiwa ni wewe umefanya kosa,omba msamaha ili maisha yaendelee kwa uzuri bila kuomba msamaha utatengeneza ufa ambao utaweza kuibomoa ndoa au kuharibu mahusiano yenu.