MAPENZI
Wanandoa wengi au waliopo kwenye mahusiano huwa wanashindwa kumaliza mambo bila ya kugombana, ni vigumu mno lakini kuna njia nyingi za kutatua au kumaliza mambo bila ya ugomvi.
1. WEKA PEMBENI KIBURI NA MAJIVUNO.
Wanandoa wengi huwa wanasumbuliwa na kiburi na majivuno au unaweza kusema kutambiana . Kiburi na Kujivuna ni vitu viwili vyenye nguvu sana kwenye ndoa ambavyo huwa vinampa mtu kujiona yeye ndiye mwenye haki mbele ya mwenzake.
2. TULIZA HISIA ZAKO.
Ni busara sana kuweka pembeni hisia zako unapokuwa kwenye wakati sahihi wa kutafuta Suluhu kwenye ndoa yako au mahusiano. Kuna mstari mwembamba kati ya kuongea ili kujenga na kuongea kubomoa na pia kwenye maongezi, msikilizaji anaweza kukutafsiri vibaya. Kabla ya kutamka jambo lipime ili lisilete ukakasi.
3. EPUKA SHUTUMA.
Mnapokuwa kwenye tofauti ni vizuri kuepusha kulaumiana hasa pale unapomtaja mwenza wako kwamba ndiye aliyefanya kosa. Suluhisho litakuja pale wote mnapokubaliana kwamba msonge mbele bila kunyoosheana vidole.
4. SIKILIZA ZAIDI ONGEA KIDOGO.
Pale unapoweza kutega sikio ndipo unapopata kiini cha tatizo na vilevile kusikia sumu alizonazo mwenzako. Ukimpa nafasi mwenzako kuongea pia unaepusha ,nyote wawili kuongea kwa pamoja kama wanena kwa lugha. Sikiliza zaidi na ongea kidogo,ina faida sana Katika kujenga Ndoa au Mahusiano imara.
5. EPUKA KUINGILIA MAONGEZI.
Pale mwenza wako anapoongea mpe nafasi aongee amalize ,anapomaliza kuongea nawe ndipo unapata pointi za kujibu kile alichosema. Ukidakia kila anachoongea mtaishia kutokuelewana. Ongozwa na busara ya kusikiliza zaidi.
6. FIKIRI KABLA YA KUONGEA.
Ni ngumu lakini inakutaka ufanye hivyo ili kunusuru kuingia kwenye tanuru la moto wa ugomvi.