MAPENZI
1. HAJASHAWISHIKA KWAMBA WEWE NDIYE.
Unapoingia kwenye mahusiano kwa mara ya kwanza ni ngumu sana kwa mwanaume kuamini kwamba wewe ni mtu sahihi kwake mpaka pale mtapokaa ,ukampa sababu ya kwamba wewe ndiye mtu wake.
2. TABIA ZAKO ZINAMFANYA AWE NA MASHAKA.
Sio rahisi kwa mwanaume kutongoza Mwanamke na haraka sana akataka kumuoa bila ya kurizika kwamba huyu ni Mwanamke wa ukweli ambaye anaweza kulea watoto na pia akawa chanzo sahihi cha furaha ndani ya ndoa.
3. KUMPA MAHITAJI KAMA MKE WAKE.
Unaishi nae ,unampikia ,unamfulia nguo zake ,unafanya nae tendo la ndoa na mambo kama hayo . Mambo haya huwa yanamfanya tayari kuamini kuwa tayari ameoa,kwenye hali hiyo ni ngumu kwenda kutoa mahari na hata kutangaza ndoa kwasababu umeshajirahisha. Lakini inapotokea ,ili apate mzigo wote ni lazima aulipie lazima atapata nguvu ya kufanya hivyo kwa haraka.
4. MWENYE WOGA WA KUOA.
Ni kweli baadhi ya wanaume wana woga wa kuoa. Unakuta mwanaume amejitosheleza kwa kila kitu lakini bado yuko pekee yake,huyu ana ugonjwa wa kuogopa kuoa. Huyu ,hawezi kukutambulisha ili mwende hatua ya pili ya ndoa.
5. AMBAYE HAYUKO TAYARI KUOA.
Unakuta kijana ana miaka mpaka zaidi ya 35 ana nyumba yake na kila kitu lakini ana wadogo zake wote wameoa. Huyu ,huenda akawa hayuko tayari kuoa . Ni mtu ambaye anatafuta ndoa yake mwenyewe ambayo haitampa majukumu ya kulea na kutunza familia, ambayo itampa uhuru wa kula bata,ndoa ambayo hatakuwa na habari na wakwe zake,ndoa ya kudumu ambayo haina migogoro. Huyu bado yupo yupo sana!
Huyu ni kama simu ya Android anahitaji kujiupdate,sasa ni wewe kumsubiri au uachane nae.
6. ANATAFUTA PESA ZAIDI.
Kwa jambo hili kuna mabinti wamewabatiza hawa jamaa jina la “mabwana pete” . Hawa huwa wanashindwa kuelewa kuwa ili uwe na ndoa yenye furaha,amani na upendo sio mpaka uwe na bilioni 5 kwenye benki.