MAPENZI
1. AMANI.
Jambo kubwa ambalo unaweza kumpa mwanaume sio mwili wako bali amani ya moyo. Hali ya hewa ambayo ataweza kuwaza vizuri,kuwa na maono sahihi, kufurahia na kustarehe. Sehemu nzuri yenye kumpa utulivu na sio shida.
Ukiona huwezi kumpa mume wako amani ebu muache mtoto wa watu endelea na mambo yako mengine.
2. UELEWA.
Mwanaume anahitaji umuelewe. Muelewe kwa mfano kwenye masuala ya kipato chake,na hapa jitahidi uishi kutokana na alicho nacho na sio kuhitaji kikubwa zaidi kupitiliza. Uelewa wa asili yake labda ni mtu mwenye hasira au ni mambo gani anapenda na yapi anachukia?
Mwanamke mwelevu ni rahisi kuuteka moyo mpaka figo za mwanaume wake.
3. HAMASA.
Mwanaume hawezi kukuomba umpe hamasa . Mwanamke maneno yako ndio yanampa hamasa, mfano “mume wangu mzuri nakupenda, nina bahati ya kuwa na Mwanaume kama wewe mpambanaji na niko nawe mume wangu kwenyejambo ili”
Maneno mazuri yanampa mwanaume nguvu ya kupambana bila kukata tamaa. Wanaume wanahitaji vitu ndio kiu yao kubwa.
4. HESHIMA.
Jishushe kwa mume wako ,usipende ushindani nae. Hakuna mwanaume anapenda kuoa mama au dada mkubwa mwenye mamlaka sawa na yake kwenye ndoa.
Katika maongezi yako ,ongea nae kwa heshima. Mpe utukufu kama ambao huwa unampa mchungaji wako wa Kanisa.
5. KUJALI.
Mwanaume anapenda kushikwa kama mtoto mchanga,anapenda kuhisi kweli yuko kwenye mazingira sahihi. Mwanaume anahitaji kujaliwa kama alivyokuwa kwa mama yake,nawe kama mama mfanyie hivyo. Mpikie chakula kizuri na hakikisha amekula na kushiba.
Huyu ndiye mwanaume wako,usione aibu kumfanyia haya yote.