NYOTA WETU
Marcus Rashford wa Manchester United alizozana na mpenzi wake Mfaransa baada ya kulewa huko Belfast, hatua iliomtoa nje ya chumba cha hoteli walikokuwa wamelala.
Siku ya Januari 25,2024 majira ya saa tisa alfajiri katika hoteli ya nyota tano huko Ireland Kaskazini, tukio hilo lilitokea . Inaelezwa kuwa Rashford alikerwa na kuzitupa nguo za Mwanamke huyo kwenye korido baada ya Mwanamke kumshutumu Rashford kwa usaliti kufuatia kumbusu Mwanamke mwingine kwenye klabu ya usiku .
Marcus Rashford mwenye umri wa miaka 26 alipanga chumba cha paundi 1,500 sawa na TSH mil 4.8 katika hoteli ijulikanayo kama Fitzwilliam huko Belfast kwa usiku mmoja na alikaa hapo kwa siku 3.
Mapema siku ya Ijumaa Rashford alirejea Manchester akiwa na usafiri binafsi wa ndege na kupiga simu saa nne asubuhi kwenye klabu yake ya Manchester United kuwa alikuwa anaumwa hawezi kuhudhuria mazoezi ya timu.
Na baada ya klabu kugundua mchezaji wao huyo alienda kujivinjari amepewa adhabu ya kupigwa faini ya paundi 650,000 ambazo ni sawa na bilioni 2 za kitanzania.