MAPENZI
1. WANAUME WOTE NI SAWA.
Kaka au ndugu yako akiwa ana tabia mbaya haimaanishi kuwa wanaume wote Duniani zaidi ya bilioni 3 wako sawa na kaka na ndugu zako. Mwanaume mzuri na mbaya unamtengenezea wewe mwenyewe.
2. WANAUME WANAPENDA NGONO NA CHAKULA.
Sio kweli, kwamba wanaume wanapenda hayo mambo na usiyape mkazo sana kwa maana kama ni chakula kinaweza kupatikana Mgahawani na kama ni ngono anaweza kuipata kwa Mwanamke mwingine. Mwanaume anahitaji Mwanamke mwenye akili.
3. WANAWAKE WANAAMINI HAWAWEZI BILA UWEPO WA WANAUME.
Mwanamke kujishusha thamani kufikia hapa,ni tatizo hata MUNGU hapendi kwasababu yeye alikuumba kwa mfano wake haijalishi juu ya jinsia yako.
4. KUPENDWA.
Wanawake wengi huwa na shauku ya kupendwa zaidi ya kitu kingine chochote lakini ukweli ni kuwa hakuna mwanaume anayeweza kukupenda kama unavyojipenda. Mapenzi pia sio kila kitu kuna vitu vingine vizuri zaidi ya kupendwa.
5. IPO SIKU ATABADILIKA.
Kama kwenye uchumba aliwahi kudhubutu kukupiga ,unawezaje kumwamini kuwa hatokupiga akikuoa? Alikuwa anakunywa na kulewa, je unamuamini vipi kuwa atabadilika? Wanawake wengi huwa wanajidanganya kwa ili.
6. KWASABABU ANA PESA BASI TUTAFURAHIA NDOA YETU.
Hata umiliki pesa zote za Dunia lakini ukikosa furaha na amani hutokaa uwe na furaha. Pesa inaweza kununua vitu lakini sio utu.