MAKALA
Baada ya siku ya leo nchi ya Namibia 🇳🇦 kufiwa na Rais wake ,Hage Geingob ni rasmi sasa Afrika imekuwa na Viongozi wakuu wa nchi ambao wamefia madarakani.
ORODHA YA MARAIS WALIOFIA MADARAKANI
1. OMARY BONGO – GABON 🇬🇦
Alikuwa ni Rais wa Gabon ,alifariki Dunia Juni 8,2009 kwa shambulio la moyo akiwa amekaa madarakani kwa takribani miaka 42.
2. UMARU MUSA YARADUA – NIGERIA 🇳🇬
Alikuwa Rais wa Nigeria alifariki Dunia Mei 5,2010 jijini Abuja akiwa na umri wa miaka 58,aliugua kwa muda mfupi.
3. MALAM BACAI SANHA – GUINEA BISSAU 🇬🇼
Alifariki Dunia Januari 12,2012 kwa ugonjwa wa kisukari akiwa na umri wa miaka 64.
4. BINGU MUTHARIKA – MALAWI 🇲🇼
Alifariki Dunia Aprili 5,2012 jijini Lilongwe akiwa na umri wa miaka 78 . Sababu ya kifo chake inatajwa ni shambulio la moyo.
5. JOHN ATTA MILLS- GHANA 🇬🇭
Alifikwa na umauti Julai 24,2012 kwa maradhi ya saratani ya koo jijini Accra ,akiwa na umri wa miaka 68.
6. MICHAEL SATA- ZAMBIA 🇿🇲
Alifariki Dunia Oktoba 28,2014 jijini London, Uingereza alipopelekwa kwa matibabu akiwa na umri wa miaka 77.
7. PIERRE NKURUNZINZA- BURUNDI 🇧🇮
Alifariki Dunia Juni 8,2020 baada ya kupatwa na shambulio la moyo akiwa na umri wa miaka 55.
8. IDRISS DEBY- CHAD 🇹🇩
Alifariki Dunia Aprili 20,2021 baada ya kujeruhiwa akiwa mstari wa mbele katika mapigano na waasi nchini Chad,akiwa na umri wa miaka 68.
9. JOHN MAGUFULI- TANZANIA 🇹🇿
Alifariki Machi 17,2021 kwa maradhi ya moyo akiwa na umri wa miaka 61 . Alifikwa na umauti akiwa hospitali ya Mzena jijini Dar es salaam.
10. HAGE GEINGOB- NAMIBIA 🇳🇦
Amefariki Dunia Februari 4,2024 kwa maradhi ya saratani akiwa na umri wa miaka 82. Amefia kwenye hospitali ya Lady Pohamba jijini Windhoek.